picha maktaba
Na Woinde Shizza,Arusha
Na Woinde Shizza,Arusha
Umoja
wa wauza nyama jiji la Arusha (wanjamuco) wametenga kiasi cha shilingi
laki tano katika mapato yao kwa ajii ya kuzilipia kaya mbili kwa kila
kata zinazoishi mazingira magumu bima ya afya ambayo itawawezesha
kupata matibabu bure katika hospitali na zahanati yeyote iliyopo ndani
ya jiji la arusha.
Hayo yalisemwa na mwenyekiti wa umoja huo wa
wafanyabiashara wa nyama Alex Lasiki alipokuwa akizungumza katika
sherehe za kuadhimisha mwaka mmoja toka kuanzishwa kwa umoja huo.
Alisema kuwa katika kusherehekea kwao mwaka mmoja wao kama
wanachama wamekubaliana kuwa watenge kiasi hicho katika mapato yao
waliyoyapata kwa mwaka mzima ili wawezeshe familia mbili zenye watu
12 zinazoishi mazingira magumu kupata bima ya afya ijulikanayo kama
lita ambayo inasimamiwa na jiji la Arusha .
Lasiki alieleza kuwa kupitia bima hiyo familia hizo
zitapata huduma za matibabu bure sehemu yeyote kwenye zahanati au
hospitali na kwamba wameamua kufanya hivyo ikiwa ni sehemu ya kurudisha
faida wanayoipata katika jamii wanayoiudumia kupitia biashara yao ya
uuzaji wa nyama.
Aidha akielezea changamoto zinazoikabili umoja huo alisema
kuwa ni pamoja na uanzishwaji wa mabucha feki ambayo hayana viwango
haswa yaliopo Samunge ambayo yamekuwa yanauza nyama ambazo hazina
viwango hivyo kuhatarisha afya za walaji.
Samba mba na hilo waliiomba pia serikali iwajangee kiwanda
cha kuchakata ngozi kwani kwa sasa wanakabiliwa na changamoto ya sehemu
màalum ya kuuzia ngozi kutokana na serikali kupiga marufuku
usafirishwaji wa ngozi hizo nje ya nchi.
Akizungumza katika maadhimisho hayo Diwani wa kata ya
Olerian Zakaria Absalum ambae pia ni mfanyabiashara wa nyama amesema
kuwa zipo kero kubwa ambazo zinawakabili wafanyabiashara wa jiji la
arusha ikiwemo usafirishwaji wa ng'ombe kwenda nchi jirani ya Kenya
ambapo wanaosafirsha hawalipi kodi na wanavyofika mpakani mtu mmoja
mwenye leseni yeye ndio analazimika kuingiza mifugo yote kwenda
kufanya biashara kwenye ardhi ya kenya bila kuilipia ushuru na hivyo
kuisababishia serikali hasara.
Alidai kuwa kutokana na kero hiyo ni vema serikali ikajenga
mnada maalum eneo la Namanga ili ijenga ushindani wa wafanyabiashra hao
ili kuziba mianya ya wale wanaoingiza mifugo bila kuwa na leseni za
biashara.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia