Mkuu wa wilaya ya Same Bi Rose Mary
Senyamule kwa niaba ya serikali amepokea madarasa 6, ofisi za walimu,
vyoo Na nyumba za walimu na mradi wa Maji kwa ajili ya wananchi ambapo ni
ushirikiano wa masista wa Grail, Joy of faith Na Korea Hope Foundation.
Bi Rose amesema madarasa hayo
yamejengwa katika kitongoji cha Endevesi, kata ya Njoro, ambapo watu
inayoishi eneo ni jamii ya kifugaji
Amesema jamii hiyo ya Endevesi
walikuwa wakipata changamoto kubwa ambapo watoto walikuwa wakitembea
umbali wa kilomita 5 kwa ajili ya kupata Elimu na kusababisha watoto wengi
kukosa shule na wengi kuwa watoro.
" Shule tumejengewa, serikali
tutahakikisha tunapanga walimu Na shule hii inaanza 2018. Wananchi hakikisheni
mnawaleta watoto shuleni. Nasi tutawachukulia hatua wote watakaokuwa
watoro."
Hata hivyo amewashukuru wafadhali
hao kwa kuunga mkono juhudi za Mh. Rais wa Tanzania katika kuhimiza elimu.