Watendaji wa mitaa pamoja na Mkurugenzi wa jiji la Arusha Katika Kikao maalum cha utendaji kazi |
Watendaji wakiwa wakimsikiliza mkurugenzi wa jiji |
Watendaji wa taka pamoja na mitaa katika halmashauri ya jiji la Arusha wameagizwa kutenga siku malum katika
wiki kwa ajili ya Kusikiliza malalamiko ya wananchi na kuyapatia utatuzi kwa
kuwa mengine yako ndani ya uwezo wao kiutendaji.
Akizungumza na watendaji wote wa Mitaa katika jiji la
Arusha Mkurugenzi Bwana Athumani Kihamia
amesema kuwa amewapa watendaji hao kila siku ya ijumaa ya kila wiki kuhakikisha
wanaiweka kwa ajili ya kusikiliza malalamiko ya wananchi na kuyajibu kwa
maandishi .
Kihamia amesema kuwa mara nyingi kumekuwa na malalamiko
mengi yanapelekwa kwa mkuu wa mkoa ,Mkuu wa wilaya ,na Mkurugenzi pamoja na
ofisi za juu ambayo yana uwezo wa kutatuliwa katika ngazi za mitaa ambayo ni
kazi ya watendaji hao.
Naye Bwana Kihamia amesema kuwa ametenga siku ya
jumatano kwa ajili ya kusikiliza malalamiko ya wananchi na kuyapatia utatuzi ili
kuwapunguzia wananchi matatizo ambayo yanauwezo kutatuliwa kwa wakati.
“Mpaka wale watu wanafika huku wanaweka foleni kwa mkurugenzi ,mkuu wa wilaya au mkuu wa mkoa nataka mje tu siku moja mtembelee muone matatizo wanayoyasema yako ndani ya uwezo wenu watendaji na ikiwezekana muweke tangazo ili wananchi wajue siku hiyo iwe maalum” Mkurugenzi Amesema Kihamia
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia