Waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Katibu Wa Halmashauri Kuu Ya Chama Cha Mapinduzi (NEC), Itikadi na Uenezi Ndg Humphrey Polepole katika Ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.
Aliyekuwa mgombea Ubunge wa Jimbo la Longido kupitia Chama Cha Mapinduzi Dkt
Steven Kiruswa akizungumza na waandishi wa habari katika
Ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar
es Salaam. Kushoto kwake ni Katibu Wa Halmashauri Kuu Ya Chama Cha Mapinduzi (NEC), Itikadi na
Uenezi Ndg Humphrey Polepole
Na Mathias Canal,
Dar es salaam
Chama cha
Mapinduzi kimesema kuwa kipo tayari kuingia katika uchaguzi mdogo wa Ubunge
Jimbo la Longido Mkoani Arusha mara baada ya kutangazwa kuwa jimbo hilo lipo
wazi kutokana na maamuzi ya mahakama ya Rufaa iliyobainisha kuwa uchaguzi wa
mwaka 2015 haukuwa huru na haki hivyo kufuta matokeo ya uchaguzi huo.
CCM imeeleza kuwa
kulikuwa na matumizi yasiyostahili kutumika kujazwa matokeo ya Ubunge, kwa
kutumia fomu namba 21c za kujaza matokeo ya Udiwani na kujaza matokeo ya
Ubunge, badala ya kutumia fomu namba 21b jambo lililopelekea kufungua kesi ya
kupinga ushindi wa Ubunge katika Jimbo hilo.
Kauli ya CCM
imetolewa na Katibu Wa Halmashauri Kuu Ya Chama Cha Mapinduzi (NEC), Itikadi na
Uenezi Ndg Humphrey Polepole wakati akizungumza na waandishi wa habari katika
Ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar
es Salaam.
Polepole alisema
kuwa vipo vyama vya siasa ambavyo kwa kawaida hulalamika kila vinaposikia
kushindwa na mahakama kwa madai kuwa hakuna haki lakini vyama hivyo kila
vinaposhinda vyenyewe husema mahakama imetenda haki.
Alisema kuwa kazi
ya mahakama ni kutumia sheria zilizopo na kuamua juu ya malalamiko ya wananchi
kwa kuhakikisha usawa mbele ya sheria kwa watu wote unatendeka hivyo maamuzi
yaliyotolewa juu ya kuwa wazi kwa Jimbo la longido ni sehemu ya maamuzi huru na
haki kwa mahakama ya Rufaa nchini.
Polepole alitoa
Rai kwa mahakama zote nchini kuendelea kufanya kazi yake vizuri kwa uhuru na
haki pasina kusikiliza kelele za watu wanaotaka mahakama kutekeleza matakwa yao
kinyume na sheria za nchi.
Kwa upande wake
aliyekuwa mgombea Ubunge wa Jimbo la Longido kupitia Chama Cha Mapinduzi Dkt
Steven Kiruswa akizungumza katika mkutano huo na waandishi wa habari alisema
kuwa pamoja na mapingamizi ya mara kwa mara katika kipindi chote tangu rufaa
ilipoanza kusikilizwa aliamua kuwa mtulivu kwa kusubiri maamuzi yatakayotolewa
na mahakama kama chombo huru nchini cha maamuzi.
Alisema kuwa kwa
mara ya nne mahakama ya Tanzania imethibitisha kuwa inaongozwa kwa mujibu wa
sheria na kujali haki ya mwenye haki ili isipotee bure.
Alisema CCM
ilifungua kesi mwanzoni mwa mwezi Novemba 2015 ikiwa ni wiki mbili tangu
kumalizika uchaguzi mkuu uliofanyika Octoba 25, 2015 ambapo mahakama kuu ya
Arusha ilibaini kwamba uchaguzi haukuwa huru na haki na kufikia June 29, 2016
hukumu ikatolewa na ubunge kutenguliwa jambo ambalo liliwafanya Chadema kukata
rufaa zaidi ya mara tatu.
Dkt Kiruswa alisema
kuwa wananchi wa Longido wamenyanyasika katika kipindi cha miaka miwili pasina
kuwa na muwakilishi wa kuwasemea bungeni hivyo maamuzi ya mahakama yataifanya
Tume ya Uchaguzi kutangaza rasmi uchaguzi mdogo na hatimaye muwakilishi
kupatikana kwa kura za haki.
Aidha, Polepole
alisema kuwa Chama Cha Mapinduzi katika muktadha wa CCM mpya Tanzania Mpya
kinaendelea kusisitiza siasa safi na kutoa uongozi bora.
Alisema siasa za
kutumia lugha isiyofaa, na Siasa za aina yoyote zenye mtazamo wa fitina hazina
nafasi ndani ya Chama Cha Mapinduzi katika kipindi hiki ambacho Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Mhe Dkt John Pombe Magufuli
anaongoza kwani amedhamiria CCM kuwa chama cha wananchi wote chenye mtazamo
chanya katika uwajibikaji.
Alitoa Rai kwa
vyama vingine nchini kufanya siasa za weledi pasina kutumia lugha za kuudhi
dhidi ya serikali na wananchi wake huku akiahidi kuwa chama chake hakiwezi
kupoteza muda kujibu porojo za hila kwani kitakuwa hakitendi haki katika
kuisimamia ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015-2020 kwa kuwaletea maendeleo
endelevu wananchi.
Polepole alisema
kuwa CCM inaamini katika majibizano ya hoja kwani chama hicho kina deni kubwa
kwa wananchi la kuwaletea maendeleo hivyo viongozi wote wa chama na wale wenye
dhamana katika dola kuendelea kuishi misingi ya CCM Mpya ya Uadilifu, Uaminifu,
Uchapakazi, Vita dhidi ya Rushwa, Vita dhidi ya ubadhilifu wa mali za chama na
mali za Umma, Unyenyekevu na kusikiliza watu.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia