Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani
Jafo akisisitiza jambo alipokuwa akizungumza na wananchi mara baada ya kukagua Kituo
cha Afya Kintinku wilayani Manyoni, Wengine ni Mkuu wa Wilaya ya Manyoni ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Ikungi
Mhe Miraji Jumanne Mtaturu na Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki (CCM) Mhe Daniel Mtuka
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa
na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Ikungi
Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakikagua chumba cha kuhifadhia maiti katika kituo cha Afya
Kintinku wilayani Manyoni.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo
akitembelea na kukagua mradi wa maji Kintinku/Lusilile wilayani Manyoni
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akimshukuru Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo kwa ukaguzi wa miradi ya maendeleo.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo
akikagua mradi wa maji Kintinku/Lusilile wilayani Manyoni
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo
akikagua chumba cha dawa katika Kituo cha Afya Kintinku wilayani Manyoni, Mwingine ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu
Na Mathias Canal, Singida
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, (Tamisemi) Mhe Seleman S. Jaffo (Mb)
amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida kuanza
haraka Mradi wa Ujenzi wa Chumba Cha upasuaji, na Ujenzi wa wodi ya kisasa.
Naibu Waziri Jaffo ametoa maagizo hayo wakati alipokuwa akizungumza na
watumishi wa kituo Cha afya Kintinku mara Baada ya
kutembele na kujionea uduni wa upatikanaji wa Huduma katika kituo hicho.
Alisema Mradi huo utaambatana na Ujenzi wa
maabara kwa ajili ya vipimo kwa wagonjwa, Ujenzi wa eneo la kuchomea taka na
Ukarabati wa eneo la kuhifadhia maiti.
Jafo ameonyesha kukerwa na ucheleweshwaji wa
kuanza Ujenzi huo licha ya serikali kupeleka fedha kiasi cha shilingi milioni
500 katika mwaka wa fedha 2017/2018 zitakazotosha kukamilisha Ujenzi wote.
Alisema katika awamu ya Pili zitatolewa fedha
kiasi cha shilingi milioni 220 zitakazotumika kununua vifaa vyote katika Chumba
Cha upasuaji na vifaa tiba kwa ujumla.
Naibu Waziri Jafo alisema kitendo Cha kuchelewa
kuanza Ujenzi huo kinachelewesha kuwapatia huduma bora wananchi ambayo
inahubiriwa na serikali ya awamu tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe
Magufuli.
"Haiwezekani Rais anatoa fedha kwa ajili ya
kuboresha sekta mbalimbali nchini ikiwemo sekta ya Afya halafu kuna watu
wachache wanashindwa kusimama vizuri fedha Hizo Jambo ambalo linapelekea
serikali kulaumiwa na wananchi" Alisema Jaffo
Katika hatua nyingine Mhe Jaffo alimuagiza
mhandisi wa Maji Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Vijijini Eng Gasto Mbondo
kutekeleza mpango wa shughuli za utoaji wa Huduma ya maji kupitia Mradi wa
kisima Cha Kintinku/Lusilile kilichopo Kijiji Cha Mbwasa (Mbwasa Well Field)
kwani eneo Hilo linaonekana kuwa na maji ya kutosha.
Akikagua mradi huo Mhe Jaffo alisema tatizo
kubwa kwa wananchi Ni pamoja na changamoto sugu ya upatikanaji Huduma za maji
hususani vijijini na kukamilika kwa mradi huo utapunguza umbali na muda
wanaotumia wananchi kutafuta maji.
Awali Mhandisi wa Halmashauri ya Wilaya ya
Manyoni Eng Gasto Mbondo akisoma taarifa ya utekelezaji wa shughuli za utoaji
wa Huduma ya maji alisema kuwa Mradi huo wa maji wa Kintinku/Lusilile
utakapokamilika unatarajia kuhudumia watu wapatao 45,417 kwa kuongeza 19.2%
kutoka 42.1% iliyopo mpaka 61.3% na utakuwa na Vituo 81 vya kuchotea maji (DPs).
Naye Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu Alisema kuwa
utekelezaji wa miradi hiyo utasimamiwa kwa karibu na ofisi yake ili kuongeza
Hamasa na tija.
Pia alisema katika Mradi wa Ujenzi wa majengo kwa ajili ya kituo Cha Afya
Kintinku asilimia kubwa ya mafundi watatoka katika Wilaya ya Manyoni ili kutoa
ajira kwa wananchi husika.
MWISHO.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia