Na Woinde Shizza,Ngorongoro
KIONGOZI wa mbio za
mwenge kitaifa Amour Hamad Amour,amewahamasisha na kuwakumbusha wafugaji
kujenga nyumba bora na kuondokana kuishi kwenye mazingira duni ambayo ni ya
umaskini.
Amesema kuwa utitiri wa mifugo isio na tija
haina nafasi hivyo akawasisitiza
kuwa na mifugo michache itakayowawezesha kuwa na maisha bora badala ya kuendela
kuishi maisha duni huku wakiwa na utitiri wa mifugo.
Amour, ameyasema hayo Septemba mosi mara baada ya kuzindua
kiwanda cha kusindika mazao yanayotokana na mifugo kinachomilikiwa na wanawake
wa kijiji cha Ololosokwani wilayani Ngorongoro,kwenye mbio za Mwenge wa Uhuru.
’’Haina maana kuwa na mifugo mingi wakati unaishi maisha
duni badilikeni fugeni mifugo michache yenye tija ili mjenge nyumba bora
muondokane na kuishi maisha duni’’alisema Amour.
Amour,amesema tajiri
namba moja duniani ni mfugaji na mkulima
hivyo wafuge kitaalamu na watanufaika na ufugaji wao na pia itawasaidia kuondokana na migogoro kati ya wakulima na wafugaji ambayo
husababisha uvunjifu wa amani.
Kuhusu raslimali za taifa amewataka wamuunge mkono Rais John
Magufuli,ambae amedhamiria kuinua maisha ya wanyonge kwa kulinda rasilimali za taifa zilizopo ndani ya hifadhi ili ziweze kunufaisha
wananchi wote .
.Akakipongeza kikundi hicho cha kina mama cha wajasiriamali,ambao
wameanzisha kiwanda kidogo cha kusindika mazao yatokanayo na mifugo ikiwemo
ngozi, pembe na katwo,ambazo hutumika kuzalisha bidhaa mbalimbali kitawezesha
kuboresha maisha ya familia zao.
Awali risala ya kikundi hicho imesema kuwa kiwanda hicho
kimefadhiliwa na Umoja wanchi za Ulaya,EU kupitia shirika la umoja wa mataifa
la elimu,sayansi na utamaduni,Unesco pamoja na halmashauri ya wilaya ya
Ngorongoro,ambayo imechangia shilingi milioni tano kwa ajili ya kuwaunga mkono.
Risala imesema kuwa
uanzishwaji wa kiwanda hicho unatoa fursa kwa wanawake kuweza kushiriki
kikamilifu kwenye shughuli za uzalishaji mali na hivyo kuboresha na kuinua
maisha ya familia zao.
Akizindua kituo binafsi cha mafuta cha Petrol,Diesel na taa
kilichopo Mjini Wasso,kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa alipokea changamoto
kutoka kwa mmiliki wa kituo hicho Fred Karangai, aliyesema kuna mafuta ya
magendo kutoka nchi jirani ya Kenya yanaingizwa kwa njia za panya hivyo
kuwaathiri wauzaji wazawa .
Amesema kuwa wao wanalipa kodi lakini wajanja hao ambao
huingiza mafuta kwa magendo hawalipi kodi hicvyo kuikosesha serikali mapato na
akaoma wadhibitiwe.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia