|
|
OFISI YA MWENYEKITI
TAHLISO
09
/ 09,3017
TAARIFA
KWA UMMA
PONGEZI ZA DHATI
KWA MHE.RAIS DR.JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI
Jumuiya ya Wanafunzia wa Vyuo Vikuu Tanzania
(TAHLISO), kwa heshima na taadhima Tunampongeza Mhe. Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania DR.JOHN POMBE
JOSEPH MAGUFULI kwa juhudi kubwa
anazoendelea kuzionyesha kwa kupigania na kuzilinda rasilimali za nchi yetu kwa
maslahi ya Taifa letu.
Ndugu Watanzania Tangu serikali hii ya awamu ya tano
chini ya Mhe.
Rais John P.Magufuli iingie madarakani
sasa inakaribia kutimiza miaka miwili (2) katika uongozi wake,hakika mambo
yaliyofanywa ni makubwa ambayo sisi sote kwa pamoja tumeyashuhudia kwa
mfano: Vita dhidi ya Dawa za kulevya, kuondoa
watumishi hewa serikalini pamoja na wenye vyeti feki, Vita dhidi ya ufisadi na
uhujumu uchumi, kufufua shirika letu la Ndege(ATC) kwa kununua ndege mbazo sasa
tunajivunia kuwa ni mali ya watanzania,Ujenzi wa Reli ya kisasa, Ujenzi wa
Mabweni ya wanafunzi katika Chuo kikuu cha Dar es salaam(UDSM),utoaji
wa ajira zaidi
ya 50,000 kwa vijana wahitimu,Kuimarisha utumishi wenye nidhamu na uwajibikaji
serikalini,Kuinua kwa kasi uchumi wa nchi yetu kimataifa,Kuboresha sekta ya
afya pamoja na kupunguza bei za madawa ya binadamu nchini na mengine mengi
yaliyoleta maendeleo ya nchi yetu
Pamoja na hayo yote Mhe. Rais John P. Magufuli
ameonyesha ujasiri mkubwa kwa kuzuia Mchanga wa madini ya dhahabu (Makinikia)
na kuunda tume ili ichunguze namna Tanzania tulivyokua tunapoteza mapato, Tume
ilionyesha jinsi tunavyoibiwa mapato ya Taifa kwa kipindi
kirefu.
Hakuishia hapo Juzi tarehe 07/09/2017 Mhe. Rais John P.
Magufuli amekabidhiwa ripoti
ya uchunguzi dhidi ya Madini ya Almas na Tanzanite iliyochunguzwa na kamati
mbili zilizoundwa na Mhe. Spika Jobu Ndugai ripoti ambayo imeonyesha jinsi
watanzania tulivyoibiwa kwa kipindi kirefu, Mhe. Rais hakusita kuwachukulia
hatua wale wote waliohusika katika kupelekea Taifa kupoteza
mapato.
Ukamataji wa madini ya Almas kwenye uwanja wa Ndege
yaliyokua yameripotiwa kuwa na thamani ya 31.4bn tofauti na uhalisia wake
ambapo kitaalamu Almas ile ina thamani ya 64bn hii ni hatua kubwa sana ya
kiukombozi wa nchi yetu ambayo iligeuka kuwa shamba la bibi kila mtu
anajifanyia anavyotaka wazungu wanatuibia wanapeleka mali zetu kwao huku
wakituachia mashimo makubwa bila kunufaika na rasilimali
zetu.
Kwa hili tunakila sababu ya kumpongeza Mhe. Rais kwa
kuwa ameonyesha Uzalendo wa hali ya juu bila kumuonea mtu haya, Bila kujali
cheo cha mtu ameonyesha namna anavyokerwa na vitendo viovu dhidi ya rasilimali
za Taifa na pia kaonyesha uchungu mkubwa wa kuzijali Rasilimali za Taifa letu
kwa vitendo huku akituonyesha mfano unaopaswa kuigwa na kila Mtanzania katika
vita hii kubwa ya kuzilinda Rasilimali zetu ambapo ni jukumu letu sisi sote kwa
pamoja kuzilinda bila haya yoyote ile kila mmoja kwa nafasi yake mahali alipo
awe mlinzi wa Rasilimali za Taifa letu.
Ndugu Watanzania Taifa letu limefikia hapa
tulipofikia kwa sababu ya baadhi ya Ndugu zetu waliopewa dhamana na serikali
katika nyadhifa mbalimbali kukosa maadili ya uongozi aidha kwa makusudi ama kwa
bahati mbaya(uzembe) wameligharimu Taifa letu na kulisababishia Taifa kupoteza
fedha nyingi ambazo zingeweza kuisaidia serikali yetu kutuboreshea maisha
yetu,upatikanaji wa Maji, ujenzi wa barabara, Utoaji elimu bure hadi Chuo
Kikuu,huduma za afya nk.
TAHLISO Tunawaomba ndugu
zetu waliopewa dhamana na
serikali hii ya awamu ya tano ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe. John Pombe Joseph
Magufuli kwa nyadhifa
mbalimbali wafanye kazi kwa bidii na kuzingatia maadili na miiko ya Kazi zao
huku wakitanguliza Uzalendo wa nchi yetu kwa maslahi ya Taifa letu bila
kuangalia maslahi yao binafsi huku wakitambua kuwa wamesomeshwa na kodi za
wanachi wa Tanzania ili kuwatumikia Watanzania kwa moyo safi na weredi
mkubwa.
Ndugu zangu Watanzania hasa vijana wenzangu tusikate
tamaa wala kukatishwa tamaa na mtu kwa haya yaliyofanyika huko nyuma tujipe
moyo na tuendelee kutiana moyo na kumuunga mkono Mhe.Rais wetu aliyejitolea kwa
moyo wa dhati kuturudishia Tanzania Mpya tunayoitamani ambayo kwa sasa
tumeishaanza kuiona Tanzania mpya tunayoitamani, pamoja na hayo tusiache
kumuombea kwa Mungu ili amlinde na kumpa
afya njema katika kipindi hiki cha uongozi wake.
NIMALIZIE KWA
KUSEMA MHE.RAIS JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI VIJANA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU
TUNAKUUNGA MKONO NA TUKO NYUMA YAKO ENDELEA KUPIGANIA
RASILIMALI ZA NCHI YETU
AMBAZO NI URITHI TOKA KWA BABU ZETU NASI TUJE KUZIKUTA NA KUWAACHIA WATOTO WETU
NAO WAFURAHIE RASILIMALI TULIZOPEWA NA
MUNGU.
STANSLAUS P. KADUGALIZE
MWENYEKITI TAHLISO 2016/2017
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia