Mkuu wa idara ya miradi ya ANSAF, Edna Lugano akizungumza wakati wa mkutano na Wadau wa kilimo na wakulima
wa mikoa ya Iringa,Njombe na Ruvuma wamenufaika utafiti uliofanywa na ANSAF kwa
kushirikia na Alliance for Green Revolution of Africa (AGRA) ambao una lengo la kutatua changamoto za wakulima wadogo wadogo kufikia kuwa wakulima wa kati ili kusaidia kukuza uchumi wa nchi na kuelewa vigezo
vinavyochangia katika upatikanaji
wa pembejeo bora kwa wakulima.
Baadhi ya washiriki walioshiriki mkutano wa kutambulisha utafiti uliofanywa na ANSAF kwa
kushirikia na Alliance for Green Revolution of Africa (AGRA) uliokuwa na lengo
la Kutambua na kuelewa vigezo
vinavyochangia katika upatikanaji
wa pembejeo bora kwa wakulima.
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Wadau wa kilimo na wakulima
wa mikoa ya Iringa,Njombe na Ruvuma wamenufaika utafiti uliofanywa na ANSAF kwa
kushirikia na Alliance for Green Revolution of Africa (AGRA) uliokuwa na lengo
la Kutambua na kuelewa vigezo
vinavyochangia katika upatikanaji
wa pembejeo bora kwa wakulima wadogo na kutathimini mfumo wa kikanuni/ kisheria
wa udhibiti wa pembejeo.
Akizungumza wakati wa
mkutano huo mkuu wa idara ya miradi ya ANSAF, Edna Lugano alisema kuwa waliamua
kufanya utafiti kwa lengo la kumkomboa mkuliwa mdogo kuondokana na changamoto
zinazomrudisha nyuma kimaendeleo.
“tunatekeleza mradi wa miaka
miwili unaolenga uimarishaji utekelezaji wa sera wezeshi za kilimo na uratibu unawezesha
upatikanaji wa pembejeo (mbegu, mbolea na viuatilifu) kudhibiti
soko na kuhamasisha upatikanaji
wake kwa wakulima wadogo” alisema Lugano
Lugano alisema kuwa utafiti
ulilenga kutazama mahitaji ya pembejeo na kiwango cha usambazaji kwa kutazama
aina chache za mazao, Ufanisi wa mfumo wa kudhibiti ubora wa
pembejeo za kilimo na jitihada zinazofanywa na serikali pamoja na wadau wengine
katika kudhibiti biashara ya pembejeo zisizo na ubora.
“Kumekuwa na malalamiko
mengi yanayohusu uwepo wa mbegu na mbolea zisizo na ubora zinazowasababishia
hasara kubwa wakulima wadogo wadogo ili kutatua changamoto hizo tumekuja na huu
utafiti unaoweka mambo mengi wazi na jinsi gani ya kutatua kero hizo” alisema
Lugano.
Aidha Lugano alisema kuwa
utafiti huo umefanywa kwenye mikoa 10 ilichaguliwa kutoka katika kanda za
kilimo na kuzingatia minyororo ya thamani pamoja wilaya mbili kila mkoa
zilichaguliwa kwa kuzingatia umbali kutoka makao makuu ya mkoa ili kuwezesha
kulinganisha uhusiano wa umbali na upatikanaji wa pembejeo.
“Mikoa ambayo tumefanya
utafiti ni pamoja Ruvuma, Kagera, Mbeya,
Morogoro, Manyara, Rukwa, Iringa, Shinyanga na Simiyu hii ndio tuliona sahihi
kufanyia utafiti kwakuwa ipo katika kanda za kilimo na kuzingatia minyororo ya
thamani” alisema Lugano
Lugano alisema kuwa
upatikanaji wa mbegu bora kimekuwa kikwazo moja wapo kwa wakulima wadogo wadogo
hasa wale ambao hawana elimu ya kilimo na kusababisha hasa kwa wakulima na
wengine kukata tamaa ya kilimo.
“Mahitaji ya mbegu kwa mwaka
nchini inakadiriwa kuwa tani 120,000. Kati ya hizo, 25% (tani 30,000)
huzalishwa na sekta rasmi, kiasi kinachosalia huagizwa kutoka nje ya nchi na
makapuni za kibiashara” alisema Lugano
Lugano alisema kuwa makisilio ya mahitaji na
upatikanaji ya viuatilifu kwa mwaka ni changamoto kutokana na kuwa usambazaji hivyo
hutegemea mahitaji mahsusi kwa eneo maalum lenye uhitaji kwa wakati maalum
“Mahitaji ya viatilifu huongozwa na Mfumo wa
‘Integrated Pesticides Management (IPM)’ Sera ya taifa ya kilimo (2013)
inahimiza menejiment sahihi ya viuatilifu ambao unazingatia kanuni za kilimo
bora zinazozingatia usalama na uhifadhi wa mazingira takriban viuatilifu vyote
vinavyotumika nchini huagizwa kutoka nje ya nchi” alisema Lugano
Naye afisa kilimo
wa manispaa ya Iringa Gerlad Mwamila aliupongeza utafiti uliofanywa na jukwa la
kilimo la ANSAF kwa kazi kubwa waliyofanya kwa kuweza kuyafumbua maeneo yenye
changamoto na jinsi gani ya kuzitatua kwa kutuwekea wazi mapendekezo yake.
"ukiangalia
utafiti huu umewakusa sana wakulima na unamanufa kwa wakulima hivyo sisi
viongozi ambao tupo serikalini tunapaswa kufikisha elimu hii kwa viongozi wetu
wa juu pamoja na wakulima ili kukuza kilimo cha wakulima wadogo" alisema
Mwamila
Mwamila alisema
kuwa serikali inatakiwa kujipanga kufanikisha zoezi la upimaji ardhi ili
kuwasaidia wakulima wadogo kulima kwa uhakika na sio kulima kwa kubahatisha
kama ambavyo saizi wanavyolima.
"kwa kweli
halmashauri zetu hazina pesa za kutosha kufanikisha zoezi la upimaji ardhi kwa
wakulima wote,lakini kama halmashuri zikifanya kazi sambamba na taasisi binafsi
tunaweza kufanikisha lengo la kumkomboa mkulima mdogo" alisema Mwamila
Kwa upande wake
afisa kilimo wa halmashuri yawilaya ya Iringa Merry Mushi alisema kumekuwa na
changamoto kwa wakulima kuuziwa pembejeo ambazo hazina ubora hivyo halmashauri
imejipanga kutatua tatizo hilo.
"mara kwa mara
tumekuwa tutoa elimu kwa wakulima juu ya kutumia pembejeo zisizo na ubora hivyo
wakulima wameanza kuelewa na kufikisha malalamiko yake kwenye ofisi za kilimo
za wilaya hiyo ni hatua kubwa sana kwetu"alisema Mushi
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia