Mkutano
huo uliokutanisha viongozi wa Klabu za Waandishi wa Habari kutoka mikoa
27 nchini unafanyika katika ukumbi wa Tanga Beach Resort mkoani Tanga.
Akizungumza
wakati wa kufungua mkutano huo ambao utafanyika kwa muda wa siku mbili
(Septemba 15 na 16,2017),Shigela alisema serikali inatambua umuhimu wa
vyombo vya habari katika maendeleo ya jamii.
“Ukitaka
maendeleo katika jamii lazima ushirikiane na vyombo vya habari,na hata
tunapoelekea katika Tanzania ya viwanda ni vyema vyombo vya habari
vihusike”,alieleza.
Alitumia
fursa hiyo kuwataka waandishi wa habari nchini kuzingatia maadili
katika kazi yao ya uandishi wa habari huku akiwaasa kujiendeleza kielimu
ili kufanya vizuri zaidi katika kazi yao.
“Vyombo
vya habari vinafundisha,vinaelimisha,vinahamasisha ,vinakosoa na
kufichua maovu na ili kutimiza haya ni vyema mkazingatia maadili
yenu,mfanye kazi kwa usawa bila upendeleo lakini pia ni vyema mkawa
wazalendo”,aliongeza.
Kwa
Upande wake rais wa UTPC,Deogratius Nsokolo alisema miongoni mwa
changamoto zinazoikabili tasnia ya habari ni uwepo wa sera na sheria
zinazobinya uhuru wa vyombo vya habari ikiwemo sheria ya Habari ya
habari ambayo baadhi ya vifungu vyake siyo rafiki kwa waandishi wa
habari.
“Tunaiomba
serikali ifanye marekebisho katika baadhi ya vifungu kwenye sheria hii
ambavyo siyo rafiki kwa vyombo vya habari”,aliongeza Nsokolo.
Awali
akizungumza katika mkutano huo,Mkurugenzi Mtendaji wa UTPC,Abubakar
Karsan alisema mkutano huo umekutanisha pamoja wadau mbalimbali wa
habari nchini na viongozi wa klabu za waandishi wa habari kutoka mikoa
27 ya Tanzania bara na Zanzibar ukifadhiliwa na SIDA.
Alisema
katika mkutano huo wajumbe wanoshiriki watafanya majadiliano mbalimbali
kuhusu masuala mbalimbali yanayowahusu waandishi wa habari. Habari na
Kadama Malunde- Malunde1 blog,Picha zote na Oscar Assenga- Tanga Raha
Blog 
Mkuu wa mkoa wa Tanga Martin Shigela akifungua mkutano mkuu wa UTPC
Mkurugenzi Mtendaji wa UTPC,Abubakar Karsan akizungumza wakati wa mkutano huo
Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilakwa akizungumza ukumbini
Rais wa UTPC,Deogratius Nsokolo akitoa hotuba
Makamu wa Rais wa UTPC,Jane Mihanji akizungumza ukumbini