Naibu Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii Eng Ramo Makani akisisitiza jambo kwa wabunge wa kamati ya Bunge ya Ardhi Maliasili na utalii mara baada ya kuwasili katika mapango ya Amboni Jijini Tanga
Wajumbe wa kamati hiyo
waakiwa tayari kuingia kwenye mapango hayo
Wajumbe wa kamati hiyo
wakiongozwa na Guide wa Mapango hayo,Athumani Mangula kuingia kwenye
mapango hayoMwenyekiti wa Kamati hiyo, Atashasta Nditiye kulia akiwa na mjumbe wa kamati hiyo,Marry Chatanda ndani ya mapango ya Amboni
Wajumbe wa Kamati hiyo
wakiwa na wakiangalia maeneo mbalimbali ya utalii kwenye mapango
hayo
Wajumbe wa kamati hiyo
wakiwa ndani ya Mapango ya Amboni Jijini Tanga
Muuongoza watalii kwenye
Mapango ya Amboni ( Guide) wa Mapango hayo,Athumani Mangula kushoto akimsikiliza
kwa umakini mjumbe wa kamati hiyo,Nape Nnauye
Muuongoza watalii kwenye
Mapango ya Amboni ( Guide) wa Mapango hayo,Athumani Mangula akiwaonyesha wajumbe
baadhi ya maeneo ndani ya mapango hayo
Muuongoza watalii kwenye
Mapango ya Amboni ( Guide) wa Mapango hayo,Athumani Mangula akisisitiza jambo kwa
wajumbe hao
Wajumbe wa kamati hiyo
wakiingia kwenye mapango ya AmboniMeneja Mawasiliano wa Tanapa ,Pascal Shelutete kushoto akimsikiliza kwa umakini moja kati ya wajumbe wa kamati hiyo wakati wakiwa kwenye mapango ya Amboni |
Aidha pia alieleza mkakati wa kuwapatia njia mbadala wananchi wanaoendesha shughuli za kibinaadamu pembezoni mwa mto zigi eneo la hifadhi ya mapango ya Amboni Jijini hapa ili kunusuru mazingira.
Mhandisi Makani alisema kuwa mpango wa serikali ni kuinua utalii wa ndani pamoja na kutoa kipaumbele katika kuboresha miundombinu kwenye vivutio vya ndani kama hatua ya kuvitangaza.
Akizungumza na waandishi wa habari eneo la mapango ya Amboni wakati akiwa kwenye ziara ya kamati ya kudumu ya Bunge, Ardhi, Maliasili na Utalii ilipotembelea hifadhi hiyo ya asili iliyopo nje kidogo mwa Jiji la Tanga.
Mhandisi Makani alizieleza changamoto zilizojitokeza kwenye ziara hiyo kuwa pamoja na uduni wa miundombinu ya barabara, ofisi ya taarifa, kutokuwepo kwa vivutio na huduma muhimu lakini pia shughuli za kibinaadamu zinazofanywa katika eneo hilo zimeonekana kuwa tishio kwenye hifadhi hiyo.
Hata hivyo alisema kuwa serikali ya wilaya na Mkoa kwa upande wake zitalazimika kuchukua hatua ikiwemo kutafuta njia mbadala zitakazofanywa na wananchi hao ili kuacha uharibifu huo huku Wizara yake ikiangalia namna ya kushughulikia changamoto nyingine.
Miongoni mwa shughuli zinazo elezwa kufanywa na wananchi kwenye maeneo hayo ni ugongaji kokoto na kilimo kazi zilizodaiwa kusababisha mmomonyoko wa ardhi nyakati za mvua na kutishia uwepo wa mapango hayo.
Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo Mwenyekiti wa kamati hiyo, Injinia Atashasta Nditiye alisema kamati hiyo itaishawishi serikali kuwa na mpango wa kuwaendeleza watumishi wa Idara hiyo ili kuwapa utaalamu wa kutosha na hivyo kuleta ufanisi zaidi.
Nditiye alisema kuwa kamati yake pia itahakikisha kuwa vivutio vyote vya asili vinatangazwa na kwamba itawashawishi viongozi wakuu wa nchi kuvitembelea vivutio hivyo na kujionea changamoto zilizopo ili kurahisisha utatuzi wake.
Naye Mkurugenzi msaidizi wa Mambo ya Kale, Digna Tillya alieleza kuwa kituo cha Amboni ambacho kinasimamiwa na Mambo ya Kale kilianzishwa mwaka 1937 na wakoloni waingereza na kwamba vivutio vingine kwa Mkoa wa Tanga vilivyoibuliwa karne ya 16 ni mji mkongwe
Tongoni.
Tillya alieleza changamoto wanazokabiliana nazo sambamba na shughuli za kibinadamu katika maeneo hayo kuwa ni uchakavu wa miundombinu ya barabara na kukosekana kwa ofisi kwa ajili ya kutolea taarifa za kituo.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia