MWIGULU NCHEMBA AZINDUA NYUMBA ZA MAKAZI YA ASKARI MAGEREZA, GEREZA KUU ARUSHA

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba(Mb) akisalimiana na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza Mkoani Arusha alipowasili katika viwanja vya Gereza Kuu Arusha katika ziara Maalum ya uzinduzi wa nyumba za makazi ya askari wa Gereza Kuu Arusha leo Agosti 28, 2017 ambapo nyumba hizo zimejengwa hivi karibuni na Uongozi wa Jeshi hilo kwa kutumia fedha iliyopatikana katika miradi ya Shirika la Magereza. Kushoto kwa Waziri ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini Dkt. Juma Malewa.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa nyumba za makazi ya askari wa Gereza Kuu Arusha, leo Agosti 28, 2017(Wa pili kulia) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini Dkt. Juma Malewa(wa tatu toka kulia) ni Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Mhe. Gobless Lema.
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini Dkt. Juma Malewa akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi kutoa hotuba fupi ya uzinduzi wa nyumba za makazi ya askari wa Gereza Kuu Arusha.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba(Mb) akitoa hotuba mbele ya Maofisa na askari wa Magereza Mkoani Arusha katika hafla ya uzinduzi wa nyumba za makazi ya askari wa Gereza Kuu Arusha. 
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba(katikati) akikagua nyumba za askari Magereza zilizojengwa kwa kutumia fedha iliyopatikana katika miradi ya Shirika la Magereza(kushoto) ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Arusha, Khamis Nkubasi.
 Muonekano wa nyumba zilizozinduliwa za makazi ya askari wa Gereza Kuu Arusha.
 Baadhi ya Maafisa na Askari wa Magereza Mkoani Arusha waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa nyumba za makazi ya askari wa Gereza Kuu Arusha. 
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini Dkt. Juma Malewa akimpongeza Mkuu wa Magereza Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Khamis Nkubasi mara baada ya uzinduzi wa nyumba hizo(katikati) ni Naibu Kamishna wa Magereza, Tusekile Mwaisabila.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba(Mb) akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo(kulia) alipomtembelea ofsini kwake leo kabla ya uzinduzi rasmi wa nyumba za makazi ya askari wa Gereza Kuu Arusha.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa na Askari ambao ni mafundi ujenzi waliojenga nyumba hizo(waliosimama) mara baada ya hafla ya uzinduzi wa nyumba hizo. Wengine walioketi ni Kamishna Jenrerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa tatu toka kushoto), wa pili kushoto ni  Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Mhe. Gobless Lema(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post