Wabunge wa Chadema, Godbless Lema na Joshua Nassari wamesema watapeleka
kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ushahidi kuhusu
madiwani saba waliojiuzulu katika majimbo yao wanaowatuhumu kupokea
rushwa ili kujiuzulu nafasi zao.
Lema ambaye ni mbunge wa Arusha Mjini, amesema leo Jumatano kuwa,
wanashukuru Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Valentino Mlowola kuwakaribisha
kupeleka ushahidi.
"Tunashukuru sana mkurugenzi mkuu wa Takukuru kutukaribisha, tutapeleka
ushahidi wetu ofisini kwake na tunaamini atafanyia kazi tuhuma hizi,"
amesema.
Amesema mbunge mwenzake wa Arumeru Mashariki, Nassari ambaye madiwani
watano katika jimbo lake wamejiuzulu amekwenda Nairobi nchini Kenya
kuonana na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ili kupata baraka zake
kabla ya kwenda Takukuru.
"Nassari amekwenda Nairobi kuonana na Mwenyekiti Mbowe ili kumweleza
tukio hili na akirudi tutakwenda naye moja kwa moja kwa Mkurugenzi Mkuu
wa Takukuru, Mlowola," amesema.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia