Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akimpa maelekezo Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya United Builders Ltd, Harshad Patel (kushoto) ambayo inajenga mradi wa bweni na ukumbi wa mihadhara katika Chuo cha Misitu Olmotonyi alipotembelea chuo hicho jana mkoani Arusha. Aliitaka kampuni hiyo iharakishe kumaliza ujenzi wa mradi huo.
Na Hamza Temba - WMU
.................................................................
Chuo
cha Misitu Olmotonyi kilichopo mkoani Arusha kimetakiwa kuboresha
taaluma na mitaala ya kufundishia iweze kukidhi mahitaji ya jamii ya
sasa na ijayo ikiwemo kujibu kero na changamoto zinazoikabili jamii
hiyo.
Agizo
hilo limetolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne
Maghembe alipotembelea chuo hicho jana kwa ajili kukagua maendeleo yake
na kuzungumza na waalimu pamoja na wafanyakazi ambapo pia alikagua
miradi mbalimbali ya maendeleo inayojengwa chuoni hapo ikiwemo ya bweni
na ukumbi wa mihadhara.
Alisema
Tanzania ya leo inahitaji wataalamu watakaojibu kero na kutatua
changamoto mbali mbali zinazoikabili sekta ya uhifadhi nchini ikiwemo ya
uharibifu wa misitu kwa njia ya uchomaji wa mkaa, uvunaji haramu wa
magogo na vitendo vya uingizaji wa mifugo kwenye maeneo ya hifadhi
nchini.
"Ni lazima muwafundishe wanafunzi wenu
uaminifu na uzalendo wa kutumia rasilimali za misitu kwa njia endelevu,
muwafundishe uhifadhi zaidi na sio uvunaji pamoja kutumia sheria
ipasavyo katika kulinda na kusimamia rasilimali hizi huku wakitambua
kuwa rasilimali hizo zikitoweka hakuna maisha kutokana na umuhimu wake
katika maisha ya binadamu" alisema Prof. Maghembe.
Pamoja na hayo, alikitaka chuo hicho
kujiimarisha zaidi katika mafunzo kwa vitendo kufikia viwango bora
vinavyotakiwa ikiwa ni pamoja na kuendeleza waalimu kitaaluma kwa
kutumia fursa mbalimbali ikiwemo za mafunzo ya nje ya nchi kwa mfumo wa
"Scholarships".
Aidha, alikitaka pia chuo hicho
kujikita zaidi katika utoaji wa huduma kwa jamii katika sekta ya misitu
pamoja na kuanzisha na kuimarisha programu mbalimbali za utafiti ambazo
pamoja na faida nyingine pia zitakitangaza chuo hicho ndani na nje ya
nchi.
Katika
hatua nyingine, Prof. Maghembe amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya United
Builders Ltd, Harshad Patel kukamilisha haraka ujenzi unaoendelea wa jengo la
bweni na ukumbi wa mihadhara chuoni hapo. Ujenzi huo upo chini ya mradi wa
ECOPRC na jengo la bweni litakua na uwezo wa kuchukua wanafunzi 100 na ukumbi
wa mihadhara wanafunzi 200.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo
hicho, Christognus Haule alisema, chuo hicho kinatoa mafunzo ya misitu
na hifadhi ya mazingira kwa ngazi ya Astashahada na Stashahada pamoja na
mafunzo ya muda mfupi. Pia kinatoa huduma za ushauri na utafiti wa
misitu na hifadhi ya mazingira.
Akizungumzia udahili wa wanafunzi
chuoni hapo alisema umekua ukiongezeka mwaka hadi mwaka ambapo katika
mwaka wa fedha 2015/2016 idadi hiyo imeongezeka kutoka 499 na kufikia
595 mwaka 2016/2017. Alisema kwa mwaka ujao 2017/2018 wanategemea kupata
wanafunzi wengi zaidi kufikia 650.
Chuo cha Misitu Olmotonyi ni chuo cha
Serikali ambacho kilianzishwa mwaka 1937 na kinasimamiwa na Wizara ya
Maliasili kwa ajili ya kutoa mafunzo ya misitu na hifadhi ya mazingira. Chuo hicho kwa sasa kina waalimu 21 wa ngazi tofauti.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya United Builders Ltd, Harshad Patel ambayo inajenga jengo la bweni na ukumbi wa mihadhara katika
Chuo cha Misitu Olmotonyi kuhusu maendeleo ya mradi huo alipotembelea
chuo hicho jana mkoani Arusha. Aliitaka kampuni hiyo iharakishe kumaliza
ujenzi wa mradi huo.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akisaini
kitabu cha wageni alipotembelea Chuo cha Misitu Olmotonyi Mkoani
Arusha jana ambapo alitoa maelekezo mbalimbali na ushauri wa kuboresha chuo hicho. Kulia ni Mkuu wa Chuo hicho, Christognus Haule.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne
Maghembe (kushoto) akizungumza na wafanyakazi wa Chuo cha Misitu Olmotonyi Mkoani
Arusha alipofanya ziara ya kikazi chuoni hapo jana ambapo alitoa maelekezo na
ushauri wa namna ya kuboresha chuo hicho.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akizungumza na
waalimu na wafanyakazi wa Chuo cha Misitu Olmotonyi mkoani Arusha jana . Kulia kwake ni Mkuu wa Chuo hicho, Christognus Haule.
Picha ya pamoja ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (wa pili kulia waliokaa) na baadhi ya wafanyakazi wa Chuo cha Misitu Olmotonyi.
Picha ya pamoja ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (wa pili kulia waliokaa) na baadhi ya waalimu wa Chuo cha Misitu Olmotonyi.
Ujenzi bweni la wanafunzi chuoni hapo ukiwa unaendelea chini ya mradi wa ECOPRC.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne
Maghembe (wa pili kulia) akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya United Builders Ltd, Harshad Patel (kulia) ambayo inajenga jengo la bweni na ukumbi wa mihadhara katika Chuo cha Misitu Olmotonyi kuhusu maendeleo ya mradi huo
alipotembelea chuo hicho jana mkoani Arusha. Aliitaka kampuni hiyo iharakishe
kumaliza ujenzi wa mradi huo.
Jengo la vukumbi wa mihadhara (Lecture Theatre) ambalo linaendelea kujengwa chuoni hapo kupitia mradi mradi wa ECOPRC.
Baadhi ya waalimu na wafanyakazi wa Chuo cha Misitu Olmotonyi wakisikiliza maelekezo mbalimbali kutoka kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (hayupo pichani) alipotembelea chuo hicho jana mkoani Arusha.
Baadhi ya waalimu na wafanyakazi wa Chuo cha Misitu Olmotonyi wakisikiliza maelekezo mbalimbali kutoka kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (hayupo pichani) alipotembelea chuo hicho jana mkoani Arusha.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia