Ticker

6/recent/ticker-posts

GAMBO:WANANCHI JITOLEENI KUJENGA NCHI YENU



Wananchi halmashauri ya Arusha wilayani Arumeru wametakiwa kujitoa katika kuchangia kujenga nchi yao kwa ajili ya maendeleo yao wenyewe  na kuachana na dhana ya kutegemea  wageni kutoka nchi za nje.

Rai hiyo imetolewa na mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo wakati akikabidhi vifaa vya ujenzi kwa Katibu Tawala wa wilaya ya Arumeru na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Arusha alivyowaahidi wananchi wa halmashauri hiyo wakati wa ziara yake ya siku tano iliyokamilika mapema wiki iliyopita.
Gambo ametoa jumla ya mifuko 700 Saruji, mabati 200, Nondo tani 2,  lita 500 za mafuta ya dizel kwa ajili ya kuendeshea mitambo, na mbao vifaa ambavyo amevikabidhi leo Ofisini kwake.
Mkuu wa mkoa huyo amesema kuwa amefikia uamuzi huo wa kuchangia  baada ya  kuridhishwa na juhudi mbalimbali zinazofanywa na wananchi kwa kushirikiana na halmashauri katika kuchangia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ndani ya halmashauri hiyo pamoja na changamoto zilizowasilishwa na wananchi kwenye mikutano ya hadhara.
Amesema kuwa imefika wakati sasa watanzania tujitolea wenyewe na kufahamu kuwa Tanzania itajengwa na watanzania wenyewe na nimethibitisha hilo baada ya kukutana baadhi ya wananchi wanachangia maendeleo yao na badhi ya maeneo bado kuna changamoto ya wananchi kujitoa katika uchangiaji wa shughuli za Maendeleo yao.
"Baadhi ya maeneo bado wananchi wanakasumba ya kuwa kila kitu kinafanywa na serikali lakini nimefanikiwa kuhamasisha wananchi wa Mateves baada ya kulalamika hawana kivuko nikawahamashisha kuchangia hochote alicho nacho  na palepale tukapata zaidi ya mifuko mia mbili ya simenti" amesema Gambo
Hata hivyo mkuu wa mkoa huyo amewataka wawekezaji na wafanyabiashara kujitoa kuchangia shughuli za maendeleo katika maeneo yao kwa kutumia sehemu ya faida wanayoipata kuirejesha kwa wanancho.
Naye Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha Dkt. Wilson Mahera ameahidi kukaa na wataslamu na baraza la madiwani na kuanza kazi ya kutrkeleza miradi iliyopewa vifaa hivyo na kuthibitisha kuwa ndani ya miezi miwili mpaka mitatu miradi hiyo itakuwa imekamilika kulingana na vifaa vilivotolewa na mkuu wa mkoa.
Aidha amemshukuru mkuu wa mkoa huyo kwa ziara yake ya kikazi aliyoifanya katika halmashauri ya Arusha ambayo kimsingi imezaa matunda kwa kuongeza nguvu kubwa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
"Kama mnavojua bajeti katika halmashauri zetu hazitoshelezi kukidhi mahitaji ya kila mtu na kuweza kutatua changamoto zote zinazojitokeza ndani ya jamii hivyo msaad huu utasaidia kupunguza sehemu ya matatizo ya wananchi wetu" amesisitiza Dkt. Mahera
Fred Mtera mwakilishi wa kampuni ya Access Image iliyotoa jumla ya mifuko 200 ya saruji amesema kuwa kampuni yao ni mdau mkubwa wa maendeleo ya mkoa wa Arusha hivyo inapohitajika uchangiaji wa shughuli ya maendeleo kampuninhiyo iko mstari wa mbele kwa kuwa inaridhishiwa na kasi ya maendeleo katika jamii.
Mkuu wa mkoa wa Arusha alifanya ziara ya siku tano na kufanikiwa  kutembelea tarafa zote tatu za  halmashauri ya Arusha na kutembelea kata zaidi ya 18 licha ya kukagua miradi ya maendeleo pia alifungua mradi wa usindikaji na uchakataji wa bidhaa za ngozi katika kijiji cha Uwira halmashauri ya Meru na kutembelea kituo v
Cha watoto cha SOS.
Aidha Mkuu wa mkoa huyo ameyataja na kuyashukuru makampuni yaliyojitoa kuchangia vifaa hivyo na kuyataja kuwa ni pamoja na kampuni ya  Bulk Ltd imetoa jumla ya nondo tani 2 ikiwa tani moja nondo za mm 12 na tani moja mm 16, kampuni ya Japan inayojenga barabara ya Tengeru -Sakina iliyotoa mifuko 500 ya Sariji, kampuni ya Access Image imetoa mifuko 209 ya saruji pamoja na Ofisi ya mkuu wa mkoa imetoa bati 200 pamoja na mbao za kuezekea nyumba za walimu.

Post a Comment

0 Comments