
"Madaktari wamefanya kazi kubwa sana kuendelea kuokoa
maisha ya Tundu Lissu na sisi tumekaa na kufikiri kwamba ni bora
tukutane ili kwa pamoja tuweze kufanya maombezi, tunajua chama chetu
kina kila aina ya watu wenye imani mbalimbali ya dini, hivyo Baraza
tumeandaa maombo maalum kwa ajili ya Mhe. Tundu Lissu na kuita 'Tanzania
National youth Prayer for Lissu' tutafanya maombi hayo ya kitaifa na
kutoa wito kwa watu wote, jambo hili si la kisiasa na wala halina sura
ya kisiasa " alisisitiza Sosopi
Aidha Sosopi amesema kuwa wanategemea kufanya maombezi hayo
siku ya Jumapili jijini Dar es Salaam maeneo ya Sinza Darajani viwanja
vya TP na kudai kwamba mpaka sasa wamefanya maandalizi yote ikiwa pamoja
na kuandika barua kwa taasisi zote za dini kuweza kufika kwa ajili ya
maombezi hayo.
Mbali na hilo Sosopi amedai kuwa kwa kuwa wanaamini jambo
hilo halina sura ya kisiasa hivyo wanatemea kuona jeshi la polisi nchini
likifika kwa lengo la kutoa ulinzi kwa raia ambao watafika kwa ajili ya
maombezi hayo na si vinginevyo.
"Naomba jambo hili lisitafsiriwe vibaya sisi kama
viongozi wa kisiasa tutakwenda pia kusikiliza maombi na si kwenda
kuongea chochote, tutakwenda uwanjani kwa sababu sisi kama CHADEMA
hatuna kanisa wala msikiti kufanya maombezi hayo ndiyo maana tunakwenda
uwanjani hapo, tunaamini hapo ni sehemu sahihi kuweza kuwakutanisha watu
wetu wote bila kujali itikadi zao" alisema Sosopi