Ticker

6/recent/ticker-posts

SERIKALI KUBORESHA SHERIA YA TAKUKURU

  Na Woinde Shizza,Arusha


Serikali  imeanza  mchakato wa kurekebisha she ria ya kuzuia na kupambana na rushwa ili kuweza kuwabana zaidi mafisadi na kuzuia mianya yote inayoashiria ulaji rushwa.

Hayo yamebainishwa na waziri wa nchi ofisi ya rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora Anjela Kairuki  katika mkutano wa kujadili maswala ya kiuchunguzi wa mali ambazo zinapatikana kwa njia ya rushwa na kuchunguza na kubaini mali hizo zilizofichwa katika nchi zingine mkutano uliyoshirikisha shirikisho la nchi nane  za Afrika Mshariki zenye taasisi za kuzuia na kupambana na rushwa.


Alisema kuwa serikali imeanza mchakato wa kurekebisha sheria hiyo na wanasubiri bunge lijalo kuiwakilisha bungeni ili liweze kujadili marekebisho hayo na  kuyapitisha.

Alisema kuwa sheriailiopo sasaivi haiwabani kabisa mafisadi  wala rushwa na  wapokea rushwa kwani faini ambazo wanapigwa watuhumiwa hawa unakuta ni ndogo kuliko kosa alilolitenda.

"Unakuta Azabu zinazo tolewa aziendani kabisa hasara imesababishwa na mkosaji  unakuta mkosaji ameleta hasara ya mabilioni ya fedha lakina analipwa fedha kidogo tu hivyo ndio maana tumeona tufanyie marekebisho ya she ria hii ili tuweze kuwabana zaidi"alisema Kairuki

Kwa upande wake mkurugenzi wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa(TAKUKURU)Valentino Mlowola  alisema kuwa kwa kipindi hichi kumekuwa na ongezeko la wananchi ambao wanatoa taarifa za watoa rushwa ,waomba rushwa pamoja na mafisadi  hii inaonyesha ni jinsi gani wananchi hawa wameelimika na wameelewa adhari za rushwa.

Alisema kuwa adi mwezi uliopita takukuru tayari ilikuwa imekusanya shilingi bilioni 45 ambayo ni saw a na asilimia 500 za fedha zilizokuwa zimefichwa katika nchi zingine na zile ambazo zimekutwa kwa mafisadi na zimetolewa kutokana na watuhumiwa waliokuwa wanatoa na  kupokea rushwa.

"Aidha pia napenda kutoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa za watuwowote ambao wamejipatia fedha zisizo halali ,wenye Mali ambazo zimepatikana kutokana na rushwa na wanapotoa wasiwe waoga kwani kunasheria ambayo inawalinda ,na pale wanapotakiwa kutoa ushaidi wasiogope kuja kwani kunasheria ambayo inamlinda mtoa taarifa "alisema Mlowola.

Naye mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya sekta binafsi Tanzania  Godfrey Simbeye alimpongeza muheshimiwa Rais Dr,John Pombe Magufuli kwa kuanzisha mahakama ya mafisadi kwani ni jambo ambalo wao kama taasisi binafsi walikuwa wakilitamani kwa kipindi cha muda mrefu.

Alisema wao wapo tayari kushirikiana name serikali ili kuweza kukomesha kabisa tatizo hili la utoaji rushwa ,upokeaji rushwa na wale wanaojipatia fedha na  Mali kwa njia ya rushwa.

 waziri wa nchi ofisi ya rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora Anjela Kairuki akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano
mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya sekta binafsi Tanzania  Godfrey Simbeye akiongea na waandishi wa habari

mkurugenzi wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa(TAKUKURU)Valentino Mlowola akiongea na waandishi wa habari

Post a Comment

0 Comments