Balozi
wa Uingereza Nchini Tanzania, Sarah Cooke akisikiliza maelezo kutoka
kwa Mratibu Elimu Kata ya Msalato Ally Swalehe juu ya mfumo wa taarifa
shuleni, ambapo mpango umetoa tablet kwa walimu wakuu na waratibu elimu
kata. Kushoto kwake ni afisa elimu Mkoa wa Dodoma, Maria Lyimo.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Msalato wakiimba wimbo wa kumkaribisha Balozi wa Uingereza Nchini alipotembelea shule hiyo.
Wanakijiji
wa Chihanga ambao walihamasika na programu ya kuinua ubora wa elimu
Nchini na kuanzisha kituo cha utayari kwa watoto wao ambao walikuwa
wanashindwa kwenda kwenye shule mama kutokana na umbali, wakicheza ngoma
ya kigogo kumkaribisha Balozi.
Balozi
Sarah Cooke akiwa na watoto wa kituo cha utayari cha Chihanga ambapo
kabla ya hapo watoto hao walikuwa nyumbani , uwepo wa kituo hicho
umewawezesha watoto kufurahia michezo mbali mbali kama vile kuimba na
kujifunza maneno ya Kiswahili ili wawe tayari kwa kuanza darasa la
kwanza. Kituo kilianzishwa mwaka jana na hii ni awamu ya pili ambayo ina
jumla ya watoto 64
Balozi akifurahia jambo na Afisa Elimu wa mkoa wa Dodoma, Maria Lyimo
Baadhi ya zana za kujifunzia watoto katika kituo cha utayari Chihanga
Balozi akikaribishwa katika kituoa cha utayari Chihanga
Watoto wa kituo cha utayari wakiwa wamejiandaa kumuimbia balozi baadhi ya nyimbo wanazojifunza kituoni
0 Comments
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia