Ticker

6/recent/ticker-posts

UWAJIBIKAJI UTENDAJI BADO UNASUASUA ZANZIBAR



Na Mwandishi Wetu,Zanzibar

Mwanaharakati natetezi  wa masuala ya demokrasia ma Haki za Binadamu
Zanzibar Ali Makame Issa, amesema dhana ya uwajibikaji katika utumishi wa
umma bado ni hafifu viswani  Zanzibar na kwamba watumishi wengi bado
wanafanya kazi kwa mazowea Visiwani humo.

Amesema utumishi wa umma , uwajibikaji,utendaji katika misingi ya uwazi,
uadilifu na ukweli hauhitaji taswira ya kuhofia muhali, kujuana, kubebana
au kuendelekeza uoendeleo na urasimu.

Tamko hilo amelitoa jana alipokua akizungumza na Waandishi wa habari mjini
Zanzibar wakati akitoa tathimini ya mkutano wa nne wa Baraza la Wawakilishi
na tokeo la kukosekana kwa upinzani katika Baraza hilo.

Alisema kuwa Zanzibar inakabiliwa na tatizo la watumishi wa umma
kufanyakazi kwa mazowea na kukosekana kwa uwajibikaji lakini Wawakilishi
wana nafasi kubwa ya kuliondoa na kulikomesha  tatizo hilo ikiwa  waatamua
na kuisimamia vizuri serikali.

Alisema kuwa wapinzani ndani ya Baraza la Wawakilishi wanabwajibu wa na
umuhimu wa kuikosoa serikali , kuielekeza na kuisimamia kwa dhamira ya
kutekeleza majukumu ya kimsingi  ikiwemo kutatua kero za wananchi pamoja na
kupambana na vitendo vyab ubadhirifu serikalini .

“Zanzibar bado usimamiaji wa kazi zake ni mdogo kwani unaweza kwenda
ofisini kufuata huduma is hasha  ukaambiwa  kuna mtu amefiwa hivyo watu
wote wamekwenda  mazikoni, wananchi wengi  wanashindwa kupata huduma kwa
wakati kwasababu ya mtendaji mmoja dhamana amefiwa.”alilalamika Issa ambaye
pia ni mwanasiasa mkongwe Zanzibar.

Alisema kwa kuwa baraza la Wawakilishi lina Wajumbe na uwakilishi mkubwa
kutoka Chama kimoja  hivyo   lazima Wawakilishi ambao si sehemu ya
serikali  wakaongeza nguvu katika ukosoaji na kusimamia ipasavyo serikali
ili kuharakisha dhana ya maendeleo kwa Zanzibar na wananchi wake baada ya
chama kikuu cha upinzani kususia uchaguzi mkuu wa marudio wa Zanzibar.

Alisema hatua ya CUF kususia uchaguzi wa marudio na kulazimika kupoteza
uwakilishi wake katika Baraza na serikalini, kumetoa nafasi pekee kwa CCM
ya kuleta mabadiliko ya kisiasa na ustawii jamii kwa wananchi wake ikiwa
Wawakilishi na serikali watadhamiria .

Alisema wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kutoka kisiwani Pemba iwapo
watafanya kazi kwa karibu na wananchi , kutatua kero zilizopo  na kuziondoa
baada ya kuwa wabunge na Wawakilishi kwa muda wa miaka 25 toka cham kimoja
kushindwa kutatua kero hizo  katika Majimbo 18 ya Pemba.

Alikosoa uamuzi na hatua ya CUF kususia uchaguzi wa marudio na kueleza
kumevuruga malengo mazima ya kufikiwa kuundwa kwa serikali ya umoja wa
kitaifa ambayo kwa namna moja au nyingine ilifanikiwa kuwaunganisha
wananchi wa Zanzibar na kujenga umoja wa Kitaifa.

“CUF wakubali kuwa wamefanya makosa yabkihistoria kwa kususia uchaguzi
warudi , wapiga kura wao wawambie na kukiri kuwa walifanya makosa na
kuwataka  radhi.”alisema Issa aliyewahi kupitia vyama vya CUF ACT Wazalendo
na ADC.

Alisema milango ya maendeleo katika kipindi cha miaka mitano ya Serikali ya
Umoja wa kitaifa ilianza kufunguka na kufufua matumaini mapya kwa wananchi
wa Zanzibar licha ya kuzuka ghasia za kiharakati, watu kumwagiwa tindikali,
viongozi wa dini kujeruhiwa na wengine kuuawa.

Hata hivyo alisema Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BLW)
wanakabiliwa na kazi kubwa ya kusimamia serikali bila ya kujali itikadi za
vyama ili kuziba ombwe na pengo la kukosekana wapinzani ili serikali iweze

Post a Comment

0 Comments