Naibu
Waziri (Ofisi ya Waziri Mkuu), Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na
Walemavu, Dkt. Abdallah Possi amelipongeza Shirika la Umoja wa Mataifa
la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) kwa kusaidia kutoa elimu kwa
wananchi kuhusu watu wenye ualbino pamoja na kufanya tathmini jinsi
wananchi walivyo na uelewa kuhusu watu hao.
Dk.
Possi ameyasema hayo katika mkutano wa kuelezea tathmini ambayo
imefanywa na UNESCO kwa wananchi wa wilaya nne ambazo tathmini
ilifanyika na kusema kuwa ni jambo zuri ambalo limesaidia kuonyesha hali
jinsi ilivyo na ni njia gani ambayo serikali inaweza kutumia ili
kumaliza vitendo vya ukatili kwa watu wenye ualbino.
"Watu
wenye ualbino wamekuwa wakiteseka kwa kipindi kirefu, wanakosa nafasi ya
kusoma, kufanya biashara na mambo mengi yanawakabili, watu wa mashirika
sio suluhisho ni jamii yenyewe, watu wengi bado hawana elimu ya kutosha
kuhusu ualbino,
"Inabidi
ifike hatua watu wenye ualbino waishi sawa na watu wengine na serikali
imekuwa ikifanya jitihada kumaliza vitendo hivyo lakini inabidi jamii
itambue hili sio jukumu la serikali peke yake ni muhimu kila mmoja
akashiriki kuvitokomeza vitendo vya ukatili, UNESCO imetuonyesha njia ya
kuiwezesha serikali kufanikisha nia yake," alisema Dkt. Possi.
Mkuu
wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCO nchini, Zulmira Rodrigues akizungumza
machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Naibu Waziri Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera,Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Mhe. Dkt Abdallah
Possi kutoa hotuba kwenye mkutano wa UNESCO unaoangalia tathmini ya watu
wenye ulemavu wa ngozi uliofanyika leo katika hoteli ya Protea
Courtyard jijini Dar es Salaam. (Habari picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog)
Kwa
upande wa UNESCO kupitia Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCO nchini,
Zulmira Rodrigues alisema UNESCO imnatambua kila mwanadamu ana haki ya
kuishi kama binadamu wengine na kupitia utafiti wao ambao uliambatana na
kutoa elimu wanaamini kuwa ni muda wa jamii kushirikiana ili kutokomeza
vitendo vya kikatili kwa maalbino.
"UNESCO
imeamua kujihusisha sana na hili jambo na kujitahidi kutoa elimu kwa
jamii, tumeanza kulifanyia kazi jambo hili la kikatili kwa maalbino na
mashambulizi ambayo wamekuwa wanakutana nayo sababu ya imani za
kishirikina ambazo ni kinyume na haki za kibinadamu,
"Utafiti
huu utaweza kusidia kumaliza vitendo vya kikatili kwa watu wenye
ualbino, kila mtu ana haki za kimsingi na hilo ndilo ambalo UNESCO
inalisimamia, na katika kufanikisha hili kila mtu katika jamii kwa
nafasi yake ana wajibu wa kushiriki kumaliza vitendo hivi, ni lazima
kushirikiana kumaliza jambo hili," alisema Rodrigues.
Tathmini
hiyo imefanyika katika wilaya nne ambazo ni Misungwi na Sengerema kwa
Mwanza, Msalala iliyopo Shinyanga na Bariadi mkoani Simiyu.
Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na
Walemavu Mhe. Dkt Abdallah Possi akizungumza katika mkutano wa UNESCO
unaoangalia tathmini ya watu wenye ulemavu wa ngozi uliofanyika leo
katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Jumuiya ya watu wenye Alibinism Tanzania (TAS) Nemes Temba akitoa
neno kwenye mkutano wa UNESCO unaoangalia tathmini ya watu wenye ulemavu
wa ngozi uliofanyika leo katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar
es Salaam.
Mhadhiri
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kiongozi mkuu wa tathmini hiyo, Dkt.
Nandera Mhando akiainisha mambo muhimu yaliyobainika kwenye tathmini
wakati mkutano wa UNESCO unaoangalia tathmini ya watu wenye ulemavu wa
ngozi uliofanyika leo katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es
Salaam.
Balozi
wa Sweden nchini Tanzania Bi. Katarina Rangnitt akitoa maoni kwenye
mkutano wa UNESCO unaoangalia tathmini ya watu wenye ulemavu wa ngozi
uliofanyika leo katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
Kulia ni Balozi wa Uturuki nchini, Yasemin Eralp.
Balozi
wa Uturuki nchini, Yasemin Eralp akizungumza jambo kwenye mkutano wa
UNESCO unaoangalia tathmini ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albinism)
uliofanyika leo katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) nchini, Dr. Qasim Sufi
akifafanua jambo wakati wa mkutano wa UNESCO unaoangalia tathmini ya
watu wenye ulemavu wa ngozi (Albinism) uliofanyika leo katika hoteli ya
Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na
Walemavu Mhe. Dkt. Abdallah Possi akifafanua jambo kwenye mkutano wa
UNESCO unaoangalia tathmini ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albinism)
uliofanyika leo katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
Picha
juu na chini ni Sehemu ya washiriki wa mkutano wa UNESCO unaoangalia
tathmini ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albinism) wakiwemo wadau kutoka
mashirika na taasisi mbalimbali uliofanyika leo katika hoteli ya Protea
Courtyard jijini Dar es Salaam.
Mshehereshaji
wa mkutano wa UNESCO unaoangalia tathmini ya watu wenye ulemavu wa
ngozi (Albinism), Mathias Herman akiendesha mjadala kwa washiriki katika
mkutano huo uliofanyika leo katika hoteli ya Protea Courtyard jijini
Dar es Salaam.
0 Comments
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia