Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe
Simai Mohammed Said (Mpaka Basi) akiwa na mgeni wake Ndg Wilfred Moshi
wakiwasili katika viwanja vya Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar,
kutembelea na kujionea shughuli za Mkutano wa Baraza la Wawakilishi
Zanzibar Ndg Wilfred Moshi ni Mtanzania wa Kwanza kupanda Mlima Mkubwa
Duniani wa Evarest ukiwa na Mita 8,848, Mtanzania huyo Ndg Wilfred Moshi
amepanda mlima huo mwaka 2012. akiwa ni Mwaafrika wa Tatu kupanda mlima huo
na mwafrika wa Pili mweusi kupanda mlima huo Duniani kwa
ukubwa.
Ndg Wilfred Moshi akiwa Zanzibar kwa
matembezi na kuangalia Utalii wa Zanzibar na kupata nafasi kutembelea
Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar kwa mualiko wa Mhe Mwakilishi wa
Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said.
Ndg Wilfred Moshi akitambulishwa kwa
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar akiwa Mgeni wa Mwakilishi wa
Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said (Mpaka Basi) akisalimia
Wajumbe wa Baraza wakati wa kutambulishwa kwake.
Mtanzania wa Kwanza kupanda Mlima Evarest
Ndg Wifred Moshi akiwa katika Ukumbi wa Mkutano wa Baraza la Wawakilishi
Zanzibar akiwa mgeni wa Mhe Simai Mohammed Said. akiwa katika sehemu ya
wageni katika ukumbi huo wa Baraza Chukwani Zanzibar.
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe
Simai Mohammed Said, akimtambulisha Mgeni wake Ndg Wilfred Moshi kwa Spika
wa Baraza la Wawakilishi Mhe Zuberi Ali Maulid, alipofika kutembelea na
kujionea shughuli za Baraza la Wawakilishi wakati wa Mkutano wake leo
asubuhi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi
Seif Ali Iddi akisalimiana na Mtanzania wa Kwanza na Muafrika wa Tatu
Duniani kupanda Mlima wa Evarest Ndg Wilfred Moshi alipofika katika jengo
la Baraza la wawakilishi Zanzibar akiwa mgeni wa Mhe Simai Mohammed Said
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi
Seif Ali Iddi, akimsikiliza Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe.
Simai Mohammed Said akitowa maelezo ya mgeni wake Ndg Wilfred Moshi ambae
ni Mtanzania wa Kwanza kupanda Mlima Evarest..
Ndg Wilfred Moshi akitowa historia yake kwa
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipofika katika
majengo ya Baraza la Wawakilishi kwa mualiko wa Mhe. Simai Mohammed Said
Mwakilishi wa Tunguu Zanzibar. akitowa historia yake ya kufanikiwa kupanda
mlima huo mkubwa duniani na kuelezea tayari ameshapanda Mlima Kilimanjaro
zaidi ya mara 100.
Ndg Wilfred Moshi akiwa katika picha ya
pamoja na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwa ajili
ya kumbukumbu yake alipofika kutembelea Baraza la Wawakilishi Chukwani
Zanzibar leo. 29-11-2016 akiwa mgeni wa Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu
Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakiwa
katika picha ya pamoja na Mtanzania wa Kwanza kupanda Mlima Mkubwa Duniani
wa Evarest Ndg Wilfred Moshi alipofika katika jengo la Baraza la
Wawakilishi Zanzibar.
Imetayarishwa na
OthmanMapara.Blogspot.
Zanzinews.com.
othmanmaulid@gmail.com
0 Comments
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia