MJUE NDEGE ANAEITWA CHOZIKwa kawaida Chozi ni ndege wanaoishi maisha ya mume mmoja mke mmoja ambapo hukaa pamoja kwenye kiota kimoja na vifaranga,kwa kawaida Chozi jike ndiye anayewajibika kujenga kiota ambako hutaga yai moja hadi mawili ambayo huyaatamia kwa siku kadhaa.
Madume hufanya kazi mbili kubwa moja ikiwa ni kumsaidia jike kuwalisha vifaranga baada ya kuanguliwa pili kubwa na muhimu zaidi ni kulinda eneo la malisho.
Chozi ndege wazuri wanaovutia wanapotembea bustani yenye maua mazuri na kuipamba kwa rangi zao nzuri.
Hapa nchini ndege hawa upatikana eneo linalozunguka Mlima Kilimanjaro,kwenye Mapori ya Akiba,Hifadhi za Taifa na maeneo yenye uoto wa asili na maua ya kutosha kwa ajili ya nta mfano Hifadhi ya Taifa ya Kitulo,Mkomazi na Kisiwa cha Rubondo,Pori la Akiba Ibanda/Rumanyika,Biharamulo na Burigi yaliopo mkoa wa Kagera,Mpanga/ Kipengere liliopo kati kati ya mkoa wa Mbeya na Njombe.

About Woinde Shizza

Mwandishi , Mjasiriamali na Mbunifu wa Mavazi. Email : woindeshizza@gmail.com , Instagram: woindeshizzablog.