Katibu Mkuu wa Chama Cha
Mapinduzi Kanali mstaafu Abdulrahman Kinana amemtumia salamu za rambi rambi Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa Tanga Ndg. Henry Shekifu kufuatia kifo cha Balozi mstaafu Mhe
Waziri Juma, kilichotokea juzi tarehe 22 Novemba, 2016 jijini Dar es salaam.
Mhe Waziri Juma ameshika nyadhifa
mbalimbali za uongozi na utumishi katika Chama na Serikali. Alikuwa Mjumbe wa Halmashauri
Kuu ya Taifa (NEC) kwa muda mrefu, Katibu wa CCM ngazi ya Mkoa, na Katibu Mkuu
wa Umoja wa Wanawake (UWT), pia amekuwa msimamizi wa ujenzi wa reli ya TAZARA,
Mkuu wa Mkoa, na Balozi wa Tanzania katika nchi mbalimbali.
Mhe. Waziri, atakumbukwa na
wanachama wa CCM kwa mchango wake mkubwa katika ujenzi na uimarishaji wa Chama
chetu, na kwamba mchango wake katika kupigania na kuleta maendeleo hapa nchini
utaendelea kuenziwa na kuthaminiwa na Watanzania.
Hakika sisi ni wa
MwenyeziMungu na kwake yeye ndio marejeo yetu.
Imetolewa na:-
Christopher Ole Sendeka (MNEC)
MSEMAJI WA CHAMA
CHA MAPINDUZI (CCM)
24.11.2016
0 Comments
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia