UN YAFANYA ZIARA CHUO CHA TUMAINI UNIVERSITY ARUSHA

 Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Hoyce Temu akitoa semina juu ya
Malengo endelevu ya umoja wa mataifa katika Chuo Kikuu cha Tumaini
University Makumira kilichopo mkoani Arusha

 Wanafunzi wakifuatilia semina
Mratibu Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa nchini Amon manyama akifafanua
jambo juu ya Malengo endelevu ya umoja wa mataifa katika Chuo Kikuu cha
Tumaini University Makumira kilichopo mkoani Arusha

Na Woinde Shizza,Arusha
Maafisa kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) wamefanya ziara ya
kutembelea chuo cha Tumaini University tawi la Arusha ikiwa ni pamoja na
kutoa semina juu ya Malengo endelevu ya umoja wa mataifa ikiwemo kufuta
umasikini,kuondoa njaa na kuhakikisha upatikanaji wa maji.Program Specialist wa UNDP ,Amon Manyama amesema kuwa Wasomi na wanafunzi
walioko vyuoni wanapaswa kuelewa vizuri malengo endelevu ya umoja wa
mataifa ili waweze kuyatimiza katika ngazi zao hasa ukizingatia kuwa
wanachuo ni Wataalamu watarajiwa,na viongozi wa kesho.Manyama amesema kuwa taasisi,mashirika na jamii pamoja na serikali ina
jukumu kubwa la kutekeleza malengo hayo ili kuondoa umasikini,kujenga
uchumi endelevu,kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano UN ,Hoyce Temu amesema kuwa vijana hususan
Wanavyuoni wanapaswa kuwa mambalozi wazuri wa kuyatangaza malengo endelevu
ya UN ili yaweze kutimia na dunia iwe ni sehemu bora zaidi ya kuishi.Hoyce amesema kuwa UN ina mpango wa kuwafikia vijana walioko vyuoni na
mitaani ili waweze kuelewa vizuri juu ya malengo 17 ya Umoja wa mataifa  na
kujua jukumu walilonalo ndani ya malengo hayo.

About Woinde Shizza

Mwandishi , Mjasiriamali na Mbunifu wa Mavazi. Email : woindeshizza@gmail.com , Instagram: woindeshizzablog.