Na Bakari
Madjeshi,Globu ya Jamii
Katika
kuhakikisha kuwa vifo vya Watoto Njiti vinapungua hapa nchini,Taasisi ya
Doris Mollel Foundation imeandaa Matembezi ya Hisani ili kukabiliana na
vifo vya watoto hao kupungua.
Matembezi
hayo yenye kauli mbiu ya "Okoa Maisha ya Mtoto Njiti" yatafanyika Visiwani
Zanzibar kutokana na Wanawake wengi visiwani humo kukabiliwa kwa asilimia
kubwa na suala hilo la Watoto kuzaliwa Njiti.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam,
Mwanzilishi wa Taasisi hiyo, Doris Mollel amesema kuwa Watoto wengi
wanakufa kutokana na kushindwa kupumua wenyewe, hivyo wao kama Taasisi
imewasukuma kusaidia suala hilo.
Dorice
ametoa shukrani kwa Wadhamini waliojitolea kuasaidia kukabiliana na
suala hilo ikiwa ikiwa ni Vodacom Foundation Tanzania, GSM Foundation,
Clouds Media Group na UTT AIMS, Michuzi Media Group na wengine
wengi.
Pia
ametoa shukrani kwa Viongozi wa Serikali kama Mhe. Angela Kairuki, Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda pamoja na Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili, Wizara za Afya Tanzania Bara na Visiwani.
Kwa
upande wake Mwakilishi wa Vodacom Tanzania, kupitia kwa Mkuu wa Kitengo cha
Mahusiano na Mwasiliano, Jacquiline Materu amesema wameamua kudhamini
Kampeni hiyo ikiwa ni fursa nzuri kuondoa vifo vya Mama na
Mtoto.
Naye
Afisa Mwandamizi Masoko na Uhusiano wa UTT AMIS amesema wanashirikiana
Doris Mollel Foundation toka mwaka Jana amesema watasaidia Kampeni hiyo ya
Okoa Mtoto Njiti kuhakikisha wanapunguza vifo vya akina mama na
Mtoto.
Muanzilishi wa Taasisi ya Dorice Mollel, Dorice Mollel
akizungumza na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini
Dar es salaam leo Novemba 16, 2016 juu ya matembezi ya hisani ya
kuadhimisha Kilele cha Siku ya Mtoto Njiti Duniani, yanayotarajiwa
kufanyika Novemba 19, 2016 Mjini Unguja Visiwani Zanzibar, ambapo Mke wa
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mama Asha Balozi ndie anaetarajiwa
kuyaongoza matezi hayo. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na
Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Jacqueline Materu na kushoto ni Afisa
Mwandamizi wa Masoko na Uhusiano - UTT AMIS, Martha
Mashiku.
Mkuu wa
Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Jacqueline Materu
akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) katika mkutano
uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Serena jijini Dar es
salaam leo Novemba 16, 2016, juu ya matembezi ya hiari yaliyodhaminiwa na
Vodacom Tanzania Foundation kwa ajili ya watoto njiti yanayotarajiwa
kufanyika Mjini Unguja, Zanzibar mwishoni mwa wiki hii. Kulia ni
Muanzilishi wa Taasisi ya Dorice Mollel, Dorice Mollel.
Afisa
Mwandamizi wa Masoko na Uhusiano - UTT AMIS, Martha Mashiku (kulia)
akielezea namna walivyoshirikiana na Taasisi ya Dorice Mollel Foundation
katika kufanikisha matembezi hayo.
0 Comments
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia