WAZEE WAILILIA SERIKALI IWAPATIA BIMA YA AFYA


 Na Woinde Shizza,Arusha
WAZEE mkoani hapa wameitaka serikali kuweka utaratibu maalum wa
kuwapatia bima ya afya kwa kundi hilo ili kuwawezesha kupata huduma za
afya kiurahisi.

Waliyasema hayo walipokuwa wakizungumza katika mkutano wa pamoja
uliwowakutanisha wazee zaidi ya miatano wa jijijini hapa mara baada ya
kukutana na mkuu wa wilaya ya arusha kwa lengo la kuwaeleza changamoto
wanazokumbana nazo.

Walisema kuwa ni vema serikali ikawatengenezea vitambulisho vya  bima
ya afya kwani mara nyingi wamekuwa wakikumbana na changamoto ya
kunyanyapaliwa pindi wanapofuata huduma mahospitalini kwani wamekuwa
wakinyanyasika sana pindi wanapohitaji huduma za kiafya .

“ili kukomesha tatizo hili la kukumbana na changamoto ya kupata huduma
za kiafya kwa haraka tunaishauri tu serikali yetu sikivu itutengenezee
bima za afya kwani pale tu tunapopata matatizo ya afya inakuwa rahisi
kupata matibabu”walisema

Aidha walisema kuwa pia ipo haja ya serikali kutoa vipaumbele kwa
wazee ikiwemo hata kuwajali kwanza kwa kuwapatia mafao kwa kila mwezi
ili kuwapunguzia makali ya maisha ambayo wamekuwa wakikumbana nayo na
ivyo kuona maisha ni magumu kwani uchumi  wa kuwaingizia vipato ni
mdogo mno ikilinganishwa na gharama ya maisha ilivyo juu kwa sasa.

Vile vile waliomba ulinzi kuimarishwa zaidi ili kuwaepusha na makundi
yanayojiusisha na mauaji ya wazee kwani wazee wamekuwa wakidhuriwa na
watu wasio na mapenzi mema nao.

Mkuu wa wilaya ya arusha Fabian Gabrieli  alisema kuwa ameamua kuwaita
wazee hao ili aweze kusikiliza kero zao na kwamba tayari ameshatoa
maelekezo kuwa ni marufuku wazee kuzagazagaa kwenye makorido  huku
watumishi wakiwa wanaangalia bila kuwapatia huduma  bali wahudumiwe
haraka kupitia dirisha la wazee ambalo lilishatengwa kwa ajili yao.

Aliongeza kuwa kwa upande wa vitambulisho vya bima ya afya tayari
ameshaagiza jiji na kuwapa miezi miwili kuhakikisha kuwa wazee wote wa
jiji hilo wanapata vitambulisho vya afya ili wapate huduma za afya
bila kuwepo kwa bugudha Ya kunyanyapaliwa.


About Woinde Shizza

Mwandishi , Mjasiriamali na Mbunifu wa Mavazi. Email : woindeshizza@gmail.com , Instagram: woindeshizzablog.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia