UMOJA WA MATAIFA WASHIRIKIANA NA FURSA KUWAFIKIA VIJANA ZAIDI YA 10000

 Timu ya wazungumzaji wa Fursa wakiwa katika picha ya pamoja na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez pamoja na Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa, Hoyce Temu.
 Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akizungumza na vijana waliohudhuria semina ya Fursa mkoani Dodoma mwishoni mwa wiki hii.
 Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Hoyce Temu akitoa mafunzo ya malengo ya maendeleo enedelevu kwa vijana wa Dodoma waliojitokeza wakati wa semina za Fursa zilizofanyika Dodoma mwishoni mwa wiki hii
Baadhi ya vijana waliojitokeza kwa wingi kuhudhuria mafunzo ya Fursa mwishoni mwa wiki hii mkoani Dodoma
 Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde akizungumza na vijana wakati akifungua semina ya Fursa iliyofanyika Dodoma mwishoni mwa wiki
 Mmoja wa wazungumzaji wa semina za Fursa, Yahaya Nawanda akizungumza na vijana kwenye siku ya pili ya mafunzo ya kilimo na ufugaji yaliyofanyika mwishoni mwa wiki hii mkoani Dodoma.
 Mwanzilishi wa Fursa , Ruge Mutahaba akizungumza na vijana wakati wa siku ya pili ya semina za Fursa zilizofanyika Dodoma mwishoni mwa wiki hii
 Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akimkabidhi mmoja wa vijana waliopata mafunzo ya Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa mjini Dodoma. Anayetazama kushoto ni Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Hoyce Temu.
Baadhi ya vijana waliopata mafunzo ya Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa mjini Dodoma wakiwa katika picha ya pamoja na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez pamoja na Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Hoyce Temu.
 


Umoja wa Mataifa umeingia ushirikiano na FURSA ili kuongeza uelewa wa malengo ya maendeleo endelevu kwa vijana zaidi ya 10,000 katika mikoa mitatu ya Dodoma, Dar es Salaam pamoja na Kigoma. 

Fursa, ambayo imekuwa ikifanyika kwa miaka mitatu iliyopita, imejikita katika kuwajengea uwezo vijana wa kuzitambua fursa katika maeneo yao wanayoishi lakini pia namna ya kutengeneza miradi na biashara kupitia fursa hizo. 

Ushirikiano wa Fursa na Umoja wa Mataifa utalenga kuwafikia vijana wanaohudhuria semina za Fursa kuelewa namna Malengo ya Dunia yanavyohusiana na maisha yao ya kila siku na wajibu wa kila kijana katika kushiriki kuyakamilisha. 
Akizungumza wakati wa kuzindua semina za Fursa mkoani Dodoma, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez alisema semina za Fursa zimeweza kubadilisha maisha ya vijana wengi na hivyo ushirikiano wake na Umoja wa Mataifa katika kufikia vijana utatoa nafasi ya vijana kuyaelewa Malengo ya Dunia. 
‘Vijana wengi wana ari ya kushiriki katika kufanikisha Malengo ya Dunia, ndio maana Umoja wa Mataifa umeamua kushirikiana na Fursa ili kuhakikisha vijana wengi zaidi wanayafahamu malengo haya lakini pia wanashiriki katika kuyatekeleza’ alisema Alvaro. 
Kwa upande wake, Mwanzilishi wa Fursa, Ruge Mutahaba amesema kwa zaidi ya miaka mitatu sasa Fursa imefanikiwa kuwafikia zaidi ya vijana milioni 5, na kuwapa mbinu na maarifa ya kuweza kutumia fursa katika maeneo yao. 
‘Tunaushukuru Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na Fursa kuwafikia vijana katika mikoa ya Dodoma, Dar es Salaam na Kigoma, ili sio tu wapate nafasi ya kupata mafunzo ya Fursa na biashara balipia mafunzo juu ya Malengo ya Dunia’ alisema Ruge

About Woinde Shizza

Mwandishi , Mjasiriamali na Mbunifu wa Mavazi. Email : woindeshizza@gmail.com , Instagram: woindeshizzablog.