Ticker

6/recent/ticker-posts

VILIO ,HUZUNI ZATAWALA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI ARUSHA BAADA YA MBUNGE LEMA KURUDISHWA MAHABUSU YA MAGEREZA YA KISONGO



Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema akiwa anapanda kwenye gariya polisi mara baada ya kulazimika kwenda mahabusu katika gereza kuu la Kisongo lililopo mkoani hapa kutokana na kuwekewa na pinganizi la dhamana
Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema akiwa anapanda kwenye gariya polisi mara baada ya kulazimika kwenda mahabusu katika gereza kuu la Kisongo lililopo mkoani hapa kutokana na kuwekewa na pinganizi la dhamana
mke wa mbunge  wa jimbo la Arusha mjini Neema Lema akiwa anaondoka mahakamani  kumsindikiza mme wake mara baada ya mahakama kuisha na lema kuamriwa kwenda mahabusu ya magereza hadi ijumaa ambapo kesi yake itatajwa tena
Na  Woinde Shizza,Arusha
Vilio na majonzi vimetawala katika mahakama ya hakimu mkazi Arusha Mara baada ya Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema kulazimika kwenda mahabusu katika gereza kuu la Kisongo lililopo mkoani hapa kutokana na kuwekewa na pinganizi la dhamana.

Hatua hiyo imekuja kufuatia mabishano ya kisheria kuhusiana na dhamana ambapo mawakili wa serikali wakiongozwa na wakili Matenus Marandu pamoja na  Paulo Kadushi kupinga dhamana ya Mbunge huyo  kutoka na kile mawakili wa serikali walichodai kuwa iwapo atapewa dhamana ataenda kuendelea kufanya mikutano  ya adhara ya uchochezi.

Aidha hoja zingine zikizotajwa na mawakili hao  walieleza mahakama hiyo mbele ya hakimu mkazi Desderi Kamugisha  kuwa uchunguzi wa kesi zingine  za uchochezi zinazomkabili Mbunge huyo zinaonyesha  alipewa dhamana ili ajirekebishe  lakini ajirekebishi na amekuwa akirudia rudia makosa yanayofanana kila Mara.

 Kwa upande wake jopo la mawakili wasomi wa upande wa mshitakiwa wakiongozwa na John Malya ,Sheck  Mfinanga ,Ahmed  Hamis  na Charles Adiel Mshitakiwa ana Haki ya kupata dhamani ukizingatia kesi inayomkabili bado uchunguzi wake haujakamilika  hivyo anahaki ya kupewa dhamana kulingana na sheria na katiba inavyo dai aidha waliongeza kuwa mtuhumiwa ni Mbunge wa bunge la Tanzania hivyo mahakama inawajibu wa kumpatia dhamana kwaajili ya kuendelea na majukumu ya wananachi ambao wamemchagua.

Waliongeza kuwa pamoja na Mbunge huyo kukabiliwa na kesi mbili ambapo alitaja kesi ya kwanza inayomkabili ni namba 440 na ya Pili ninamba  441 za mwaka 2016 ya kutoa lugha  ya  uchochezi dhidi ya muheshiwa Rais ambapo alisema maneno  kuwa nchi hii aita tawalika na  itaingia kwenye machafuko iwapo Rais atafuata katiba na  sheria  hivyo bado anaamini makosa hayo yanastaili kupata dhamana kama sheria ya makosa ya mwenendo ya jinai .

Baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili hakimu kamugisha alihairisha  shauri hilo adi November 11 itakapo kuja kutajwa tena na kutolewa uwamuzi mdogo iwapo mshtakiwa Lema atapata dhamana au Ataendelea kukaa kizuizini .

Wakati Mbunge huyo akiondoshwa mahakamani hapo chini ya ulinzi mkali wa polisi  Lema alionekana kujiamini huku akiwa ameshika biblia takatifu  ndipo wafuasi wa chama cha demokrasia na maendeleo  Chadema waliangua vilio na mayowe huku wakilia Mbunge huyo.

Akitoa tamko Mwenyekiti wa chadema mkoa wa Arusha  Amani Golugwa aliwaomba wananchi wa Mkoa wa Arusha kuwa wavumilivu katika kipindi hichi kigumu cha Mbunge wao kushikiliwa na kuwataka kujitokeza kwa wingi  mahakamani kufatilia mwenendo wa kesi ya Mbunge wao.

Awali kabla  ya kuanza kusikiliza kesi hiyo jaji Salma  Majimbi alimuamuru mwanasheria wa serikali  kumleta mshitakiwa Lema  ndani ya nusu saa mahakamani hapo ,baada ya kukaa mahabusu ya polisi ndani ya masaa 175  kinyume cha she ria ya makosa ya jinai.

Post a Comment

0 Comments