Makamu
Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Bw. Hebron Mwakagenda akitoa mafunzo
kuhusu katiba ya zamani pamoja na katiba mpya kwa vijana kutoka wilaya
zote za jiji la Dar es Salaam leo. (Picha na Geofrey Adroph)
Mwenyekiti
wa Jukwaa la Katiba Tanzania Bw, Deus Kibamba akitoa elimu kuhusu
mchakato wa mabadiliko ya Katiba pamoja na historia ya mchakato huo kwa
vijana wa wilaya zote za jiji la Dar Es Salaam.
Katibu
Mtendaji wa TYVA, Saddam Khalfan akitoa ufafanuzi kuhusu shirika hilo
na madhumuni ya mjadala wa katiba na vijana uliyofanyika katika ukumbi
wa Blue Pearl jijini Dar Es Salaam
Mbunge
wa Viti Maalumu, (CUF), Riziki Lulida akizungumzia changamoto
wanazozipata kama wabunge wenye ulemavi katika katiba pamoja na kutoa
maoni kuhusu uundwaji wa katiba mpya
Mbunge
wa Viti maalum Pemba-Zanzibar, Mheshimiwa Zainabu Mussa Bakari
akizungumzia Haki na Wajibu wa mwananchi Kikatiba wakati wa ufunguzi wa
Kongamano lililowashirikisha vijana mbalimbali kutoka wilaya tano za
jiji la Dar es Salaam ili kujadili katiba mpya lililoandaliwa na Taasisi
ya Vijana ya TYVA pamoja na IRI.
Mbunge
wa Viti Maalum mkoa wa Dar es salaam Salma Mwasa (CUF) akizungumza na
vijana kuhusu balaza la vijana katika katiba inayopendekezwa ili kuweza
kuleta utatuzi wa matatizo tyao ili serikali iwasikie wakati wa
kongamano lililowakutanisha vijana kutoka katika wilaya mbalimbali za
jiji la Dar.
Baadhi ya vijana wakichangia mada
Baadhi
ya Vijana wa wilaya ya mbalimbali za jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye
mafunzo kuhusu mchakato wa mabadiliko ya Katiba yaliyofanyika leo ambao
wameazimia kuendelea kwa mchakato wa kupatikana kwa katiba mpya.
0 Comments
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia