JOH MAKINI :SIFANYI MUZIKI MZURI KWA KUANGALIA KUJA KUWA NOMINEES KWENYE TUZO

Joh Makini ameweka wazi kuwa hafanyi muziki mzuri kwa kuangalia kuja kuwa nominated kwenye tuzo flani.
 
Joh Makini
Rapa huyo kutoka kwenye kundi la Weusi, amezungumza hayo baada ya kuwepo kwa maswali mengi kuwa mbona hajatajwa kuwania Tuzo za kimataifa zikiwemo MTV kwa mwaka huu ilihali akiwa na ngoma kali kama Don’t Bother aliyo mshirikisha AKA kutoka Afrika kusini.
Lakini pia Joh ameweka wazi kuwa juhudi zake sio muziki wa Afrika Mashariki tu, Ni muziki wa Dunia na ana amini amefanya vitu vichache sana japokuwa watu wanaona amefanya vitu vikubwa huku yeye akipanga kufanya muziki mzuri zaidi na mkubwa.
Tutarajie makubwa mengi kutoka kwa Rapa Joh Makini kwenye muziki wake.

About Woinde Shizza

Mwandishi , Mjasiriamali na Mbunifu wa Mavazi. Email : woindeshizza@gmail.com , Instagram: woindeshizzablog.