Ticker

6/recent/ticker-posts

TRUMP AMSHINDA HILLATY CLINTON KATIKA UCHAGUZI WA URAIS ULIOKUWA NA USHINDANI MKALI


Donald Trump amemshinda Hillary Clinton katika matokeo ya uchaguzi wa urais uliokuwa na ushindani mkali.Hillary Clinton and Donald Trump
Donald Trump amemshinda Hillary Clinton katika matokeo ya uchaguzi wa urais uliokuwa na ushindani mkali.

Bi Clinton amempigia simu Bw Trump kumpongeza kwa ushindi wake. Rais Obama pia amempigia simu kumpongeza na kutangaza kwamba amemwalika ikulu ya White House siku ya Alhamisi washauriane kuhusu shughuli ya mpito.
Bw Trump, aliyeeleza nia yake ya kuwafanyia kazi Wamarekani wote atakapoingia madarakani, ataapishwa kuwa rais tarehe 20 Januari mwaka 2017.
Mgombea huyo wa Republican, alishangaza wengi kwa kushinda majimbo mengi muhimu na kujiweka katika nafasi nzuri ya kushinda.
Alishinda majimbo ya Ohio, Florida, na North Carolina, ingawa Bi Clinton alishinda Virginia.
Bw Trump alijizolea kura 278 za wajumbe na Clinton 218 kwa mujibu wa makadirio ya ABC News. Mshindi anahitaji kura 270 za wajumbe.
Bw Trump alishinda majimbo mengi ya kusini mwa Marekani naye Bi Clinton akashinda majimbo ya kaskazini mashariki mwa nchi hiyo, kwa mujibu wa makadirio ya shirika la utangazaji la ABC News.

Post a Comment

0 Comments