WAMTAKA RAIS MAGUFULI KUONGEZA JUHUDU ZA KUPAMBANA NA MAFISADI

Image result for WAISLAMU
Picha na maktaba

Na Woinde Shizza,Arusha
BAADHI ya viongozi wa dini ya kiislamu wamemshauri Rais  John Pombe Magufuli  kuongeza  juhudi za kupambana na mafisadi wanaomkwamisha katika utawala wake ili tanzania iweze kuwa nchi ya maendeleo na ya viwanda.

Aidha viongozi hao wamempongeza pia Rais Magufuli kwa kipindi cha uongozi wa mwaka mmoja kupambana na mafisadi na kuweza kuziba mianya ya ukwepaji kodi na rushwa na hivyo kuwepo kwa mabadiliko makubwa kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti  leo katika kongamano la kuombea nchi amani pamoja na kumwombea Rais Magufuli kwa kutimiza mwaka mmoja katika uongozi wake  viongozi hao walisema kuwa watanzania wote wanapaswa kuungana kumwimbea rais ili aendeleze mapambano ya kuthibiti mafisadi.

Katibu mkuu baraza la kiislamu la madrasat qamariyah islamiyal  kutoka temeke jijini dar es salaam shehe Rajabu Mluguta alisema kuwa wameamua kuungana kwa pamoja viongozi wa dini kutoka mikoa ya tanga,zanzibar ,tabora,shinyanga na dodoma na arusha ili kuiombea nchi na kuweza kumwombea magufuli kwani kwa mwaka mmoja wa uongozi wake ameleta mabadiliko makubwa sana.

Alisema kuwa wanachomtaka Rais Magufuli kwa sasa ni kuongeza juhudi za mapambano dhidi ya wale wanaombeza katika utawala wake huku akitolea mfano ndege mbili alizonunua siku chache zilizopita kuwa wapo watu waliosema amenunua bajaji hali ambayo alisema kuwa hizo ni kauli za kubeza na anatakiwa kuongeza mapambano zaidi.

"Sisi kama waumini wa kiislamu tunampongeza sana Rais Magufuli maana mwaka mmoja tu kuweza kununua ndege mbili ni hatua kubwa sana na natoa maoni yangu kama kiongozi wa dini aendelee kupambana na wanaomkwamisha ili maendeleo yapatikane kwa harska"aliongeza shehe rajabu.

Naibu msaidizi wa baraza hilo la kiislamu la madrast Abdulrahaman  bin musa alisema kuwa swala la amani sio lq mtu mmoja ni la watu wote hivyo kwa kipindi hiki cha mwaka mmoja kilicholeta mabadiliko kwa muda mfupi watu wote wanapaswa kumwombea rais magufuli ili akamilishe yale yote aliyohaidi kwa watanzania.

"Maendelleo hayawezi yakaja kwa kasi yenyewe ila tunamwomba yale yote aliyoaidi ayatekeleze kwa vitendo ingawa ameshatuonyesha mafanikio makubwa sana ikiwemo kuthibiti wakwepa kodi na wabadhirifu wa nchi lakini akumbuke zile ahadi alizozitoa ili mpaka anapomaliza miaka mitano tuwe tanzania ya viwanda kama alivyosema"alisisitiza

About Woinde Shizza

Mwandishi , Mjasiriamali na Mbunifu wa Mavazi. Email : woindeshizza@gmail.com , Instagram: woindeshizzablog.