Ticker

6/recent/ticker-posts

MPANGO:HALI YA UCHUMI TANZANIA NI NZURI


  Waziri wa  fedha na mipango   Philip Mpango akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano wa 18 wa taasisi za fedha
  Gavana wa Bank kuu   Benno Ndulu akiongea na waandishi wa habari 




 Mkurugenzi  Mtendaji wa CRDB Dkt. Charles Kimei akitoa hutuba katika mkutano huo






Na Woinde Shizza,Arusha

PAMOJA na  mtikisiko wa uchumi nchini Waziri wa  fedha na mipango   Philip Mpango amejitokeza na kusema hali ya uchumi Tanzania ni nzuri.


Aliyasema hayo  leo jijini Arusha  wakati akifungua mkutano wa 18 wa taasisi za fedha nchini ulioandaliwa na BOT Arusha wenye lengo la kuzungumzia namna ya kutumia fursa za kijografia katika kukuza uchumi.


Mpango alisema hali ya uchumi siyo mbaya bali  watu ndio hawataki kufanya kazi na waliozoea kupiga dili nyepesi ndio wanalalamika ila serikali haina tatizo hilo.

" Hata kama liwe taifa gani  halikosi changamoto hivyo na sisi ni  jambo la kawaida hata watu wa uchumi wanazidi kupima bado taifa letu haliko vibaya" Alisema .

" hali ya uchumi inaenda  vizuri tukiangalia sekta za fedha, deni la taifa, na hali ya chakula ipo  vizuri   tufanye kazi waliozoea dili nyepesi ndo wanaolalamika " aliongeza.

Aliagiza taasisi za fedha nchini kukopesha katika sekta za Kilimo ili kuchochea sekta hiyo kufanya vizuri.

Alisema pia ni vyema wakulima wakapatiwa elimu pamoja na mikopo yenye riba nafuu ili sekta hiyo iweze kuzalisha zaidi.

Alisema  awali serikali ilitoa  maagizo  kwa taasisi hizo  kuhakikisha wanaiangalia sekta ya kilimo kwa ukaribu  katika mikopo  ili iweze kuzalisha na nchi iwe na maendeleo kupitia sekta hiyo.

Naye Gavana wa Bank kuu   Benno Ndulu Alisema lengo la mkutano huo ni kuzungumzia jinsi gani taasisi za kifedha zitatumia fursa za jografia kuhakikisha uchumi unapanda.

Alisema changamoto inayosababisha washindwe kukopesha sekta ya kilimo ni kutolipwa fedha zao kwa wakati na wakulima hivyo wanahofia kuwakopesha.

" Tatizo linalofanya tushindwe kukopesha ni kutokana navigezo vya watu Kushindwa kurejesha mikopo" alisema Ndulu.

Hata hivyo alisema watawapatia elimu na kuwaweka  karibu ili wawapatie mikopo hiyo.

Sambamba na hayo Mkurugenzi  Mtendaji wa CRDB Dkt. Charles Kimei alisema wanaunga mkono kauli ya Serikali ya kutaka kuelekeza  nguvu kubwa ya mikopo katika sekta ya kilimo na wapo tayari kuifanyia kazi.

Post a Comment

0 Comments