WANAWAKE MKOANI MWANZA WATAKIWA KUHUDHURIA KONGAMANO LA SAUTI YA MWANAMKE.

Na George Binagi-GB Pazzo @BMG
Wanawake mkoani Mwanza wamehimizwa kuhudhuria Kongamano la Sauti ya Mwanamke litakalowakutanisha baadhi ya wanawake waliofanikiwa kiuchumi nchini, ili kujifunza na kuhamasika katika kujikwamua kiuchumi.

Mwandaaji wa Kongamano hilo, Mboni Masimba ambaye pia ni mtangazaji wa kipindi cha runinga cha The Mboni Show, amesema kongamano hilo limelenga kuwahamasisha wanawake kufanya kazi kwa bidii na kwa kujiamini zaidi bila kuongopa vikwazo vya kibiashara.

“Njoo ujifunze nguvu ya mwanamke katika biashara, kushinda vikwazo, kujiamini, kufanya kazi kwa bidii, kutoogopa hatari za kibiashara pamoja na kuwa na malengo ya muda mrefu ambapo wahamasishaji na wafundaji mbalimbali watakuwepo”. Amesema Masimba na kuongeza kwamba pia kutakuwa na burudani ya muziki kutoka kwa Isha Mashauzi na Zarry Edosha pamoja na vichekesho kutoka kwa Katarina Wa Karatu.

Aidha Masimba amesema tayari tiketi za kongamano hilo litakalofanyika tarehe sita mwezi huu kwenye ukumbi wa Gold Crest Hotel Jijini Mwanza zimeanza kuuzwa kwa shilingi elfu arobaini katika maeneo mbalimbali ikiwemo Gold Crest Hotel, TSN Super Market Rock City Mall, Flora Salon, Kayvies Beaty Parlour Magnum Hotel Ghana, Idda Garments Ghana, Diamond Bar Kona ya Bwiru pamoja Bladict Classic Wear mtaa wa Uhuru Dampo.

About Woinde Shizza

Mwandishi , Mjasiriamali na Mbunifu wa Mavazi. Email : woindeshizza@gmail.com , Instagram: woindeshizzablog.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia