UVCCM YAMGEUZIA KIBAO MBUNGE WA JIMBO LA SIMANJIRO JAMES OLE MILYAImage result for JEMSI MILYA
Katika picha ni mbunge wa simanjiro James Milya (picha na Maktaba)
Na Woinde Shizza , Manyara

Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umesikitishwa na
malalamiko ya kupika  yaliotolewa na Mbunge wa jimbo la  Simanjiro
James Milya  (Chadema) dhidi ya Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu
Shaka kudai amefanya mkutano hadhara wakati kiongozi huyo  amezugumza
na wanachama wa CCM  kwenye ofisi za chama cha Mapinduzi.

Pia Umoja  huo umesema anachoonekana kukilalamikia na kukihofia Milya
ni kujaribu kwake kujikoasha mbele ya wananchi baada ya kuona kazi
aliyoiomba ya kuwawakilisha  wananchi Simajiro ikionekana kumshinda ma
kujikuta akijitisha kwa kivuli chake .

Msimamo huo umetolewa juzi  na Katibu wa UVCCM Wilaya ya Simajiro
Bakari Mwacha alipoungumza na waandishibwa habari ofisini kwake mjini
Simanjir baada ya kimuona Mbunge wa jimbo hilo akilalamika katika
baadhi ya vyombo vya habari akimsakama Shaka kwa madai aliyoyaita ni
uongo na uzushi.

Mwacha alisema kiongozi yeyote wa chama cha siasa ana haki ya kukutana
na  wanachama wake kwenye viakao vya ndani ili  kubadilishana mawazo,
kupeana taarifa ilibkujua maendeleo na uhai wa chama na mwenendo wake
bila kuzuiwa na sheria.

"Shaka alikutana na wanachama wa CCM  katika ofisi za UVCCM wilaya
Simanjiro, akizindua jengo jipya la ofisi ya UVCCM kabla ya kufungua
mashina ya wakereketwa katika kata za Naberere na Emboret , hakutubia
mkutano wa hadhara, hatukuomba kibali polisi kwasababu ni mikutano ya
ndani "alisema Mwacha.

Aidha Katibu huyo wa UVCCM alisema alichokifanya Shaka katika ziara
yake ya siku mbili wilayani simanjiro  kinafanana na kinachofanywa na
wajumbe wa kamati kuu ya Chadema akiwemo Waziri Mkuu Mstaafu Edward
Lowassa na Feredrick Sumaye wanaozunguuka na kuzungumza na wanachama
kwenye ofisi za Chadema.

Mwacha alisema hata Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba na
Katibu Mkuu wake  Maalim Seif Sharif Hamad ambao wako katika mvutano
wa madaraka hukutana na wanachama wao hivyo si uchuro wala ajabu kwa
Shaka kukutana na wanachama wa CCM mahali popote katika vikao vya
ndani

Alisema Sumaye na Lowassa wanaongoza timu za makada wa chadema
kufanya mikutano ya ndani wakikutana na wanachama wao kwenye ofisi zao
kwa lengo la kujiimarisha kisiasa kama ambavyo Shaka na viongozi
wenzake wanavyofanya katika mikoa mingiine.

Akifafanua zaidi, Mwacha alisema UVCCM katu hawawezi kukiuka agizo na
amri ya Serikali kuhusu zuio la kutofanyika  mikutano ya hadhara
wakati huu ambao wananchi wanatakiwa kufanya kazi za uzalishaji mali
maeneo ya kazi, viwandani na mashambani.

"Milya anatafuta mtu wa kufa naye kisiasa baada ya kubaini amekwaa
kisiki  , siyo siri, wakati ukiwadia katika uchaguzi mkuu wa mwaka
2020, ima fa ima atanyanyuliwa juu kwa juu na wananchi ikiwa
hatawatumikia kama alivyowahidi mwaka 2015 " Alisisitiza Mwacha .

Mara baadavyabziaravyavShaka , Milya alionekana katika baadhi ya
vyombo vya habari akimlalamikia kiongozi huyo kwa kuingia jimboni
mwake na kufanya mikutano ya hadhara huku  akiwahamasisha wananchi na
kutaka  Milya afungishwe virago ifikapo mwaka 2020  na wananchi .

Hata hivyo Katibu huyo wa UVCCM  wilaya Simanjiro alisisitiza kuwa
viongozi wa UVCCM wataendelea na fatiki ya kufanya siasa na mikutano
ya ndani yenye lengo la kukutana na wananchi bila kuhutubia  mikutano
ya hadhara.

Simu ya Shaka iliita mara kadhaa bila kupokewa kwa  minajili ya
kutakiwa ajibu madai ya Milya kwamba aliingia jimboni mwake na kufanya
mikutano ya hadhara wakati akiwa si Diwani wala Mbunge katika wikaya
ya Simanjiro Mkoani humu .

About Woinde Shizza

Mwandishi , Mjasiriamali na Mbunifu wa Mavazi. Email : woindeshizza@gmail.com , Instagram: woindeshizzablog.