KIGWANGALA :SERIKALI KUAJIRI MAAFISA USTAWI WA JAMII WOTE NA KUWAPELEKEA KUFANYA KAZI KATIKA VIJIJI NA KATA

  Naibu Waziri Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Hamis Kigwangalla Akiwa anamtunuku mmoja wa mwanafunzi wa shahada ya uzamini  aliyejulikana kwa jina la Anna 
  Baadhi ya Wanafunzi waliohitimu fani za astashahada, shahada ya kwanza na stashahada ya uzamili ya maendeleo ya jamii katika chuo cha Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tenguru wakiwa wanajiself na naibu waziri mara baada ya mahafali hayo kumalizika
 wanafunzi waliofanya vizuri zaidi shuleni hapo waliosimama nyuma wakiwa katika picha ya pamoja na naibu waziri pamoja na bodi ya chuo hicho


 Naibu waziri akiongea na waandishi wa habari  mara baada ya mahafali kumalizika wa kwanza kulia ni  Mkuu wa Tasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru Anatory Bunduki wakwanza kushoto ni kaimu  mwenyekiti wa bodi  ya taasisi hiyo Dr,Rosemarie Mwaipopo
 wahitimu   wakiwa katika nyuso za furaha


Na Woinde Shizza,Arusha 

  Serikali inajipanga kuajiri maafisa ustawi  wa maendeleo ya jamii 5,554 kwakipindi cha miaka mitano ili waweze kutoa huduma za maendeleo ya jamii kuanzia  ngazi ya kata na  vijiji kama ilivyokuwa kwa utawala wa awamu  ya kwanza nchini 


Hayo yameelezwa na Naibu Waziri Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Hamis Kigwangalla alipokuwa akihutubia katika  mahafali ya sita  katika fani za astashahada, shahada ya kwanza na stashahada ya uzamili ya maendeleo ya jamii katika chuo cha Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tenguru nje kidogo ya jiji  la Arusha

Alisema kuwa  serikali ya awamu ya kwanza ilikuwa na idadi kubwa ya mabibi na mabwana maendeleo ya jamii kila kata hivyo ilisaidia kuwaletea maendeleo wananchi kwa haraka zaidi na kutoa ushauri wa miradi mbalimbali inayowazunguka wananchi haswa wa vijijini.

“katika serikali  ya awamu ya kwanza maafisa ustawi wa jamii walikuwa wapo hadi vijijini unakuta bibi ustawi wa jamii na babu ustawi wa jamii kitu ambacho kwa kipindi cha nyuma hapa kilipotea kabisa sasa serikali hii ya awamu ya tano tunataka kurudisha icho kitu”alisema Kigwangala

 Alivitaka vyuo mbalimbali vinavyofundishia kozi ya ustawi wa jamii kuakikisha  wanaongeza idadi ya wataaalamu wanaosomea ustawi wa jamii ili  kuweza kupunguaza tatizo hili kwani kwa sasaivi kadri siku zinavyozidi kwenda ndivo wanafunzi wanaosomea ustawi wa jamii wanapungua

“ kwasasa wataalamu katika sekta ya maendeleo ya jamii  wameanza kupungua sana na ivyo  kila  chuo  kinatakiwa kuongeza idadi ya  wa wanafunzi ili kuendana na azima ya serikali ya kuwa na wataalamu wa maendeleo ya jamii  kila wilaya , kata na hata kijiji.


Kigwangala  alitoa wito kwa  Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru kuendela kutoa elimu  yenye viwango  bora na wazingatie  katika mchakato wote wa utoaji mafunzo kuanzia kwenye udahili wa wanafunzi wenye sifa na vigezo ili kujenga jamii ya wasomi wenye tija katika Taifa letu. 
" napia napenda kusema kuwa hao wamaafisa ustawi wa jamii wasome kabisa wakijua serikali itawaajiri sawa lakini wasitegemee watakaa ofisini tu au katika ofisi za halmashauri apana wajue kabisa wataenda kufanya kazi vijijini ili waweze kutambua matatizo ya wananchi na kuyatatua pamoja nakuvumbua miradi mbalimbali ya jamii itakayosaidia wananchi "alisema Kigwangala
 Alisema Nchi itabadilika sana na kuwa na maendeleo ikiwa wanataaluma wa Nchi hii wataipenda Nchi yao kama ambavyo kila mtu ampendavyo mama yake nakujituma sana katika utendaji kazi utaendana na falsafa ya hapa kazi tu.

Kwa upande wake Mkuu wa Tasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru Anatory Bunduki akisoma hutuba wakati  Mahafari hayo alisema  kuwa pamoja na mikakati iliyopo ya kuboresha chuo hicho kwasasa chuo kimeanzisha kituo cha taifa cha utafiti na uhifadhi wa machapisho ya wanawake Nchini kituo ambacho kimeanzishwa kwa ushirikiano wa UNESCO na UNFPA pamoja na Wizara ya Afya, Maendeleo jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Alisema kuwa  lengo la kuanzishwa kwa kituo hicho ni kufanya tafiti za kina kwa masuala ya wanawake, jinsia, watoto wa kike ili kuwainua kiuchumi, kisiasa,kiutamaduni na kijamii na kuzitumia tafiti hizi kujadili katika kuandaa sera na kutoa maamuzi yanayojumuisha amsuala ya kijinsia katika kutekeleza sera mbalimbali hapa Nchini.


 Wakwanza kushoto ni mkuu wa taasisi ya maendeleo ya jamii Tengeru Anatory Bunduki akiteta jambo  na  Naibu waziri Kigwangala
 maandamano yakiwa yanaingia katika eneo la shule kwa ajili ya mahafali


baadhi ya walimu wakiwa katika maandamano hayo

About Woinde Shizza

Mwandishi , Mjasiriamali na Mbunifu wa Mavazi. Email : woindeshizza@gmail.com , Instagram: woindeshizzablog.