TANGAZO LA MAHAFALI KUTOKA TAASISI YA MAENDELEO YA JAMII TENGERU   TAASISI YA MAENDELEO YA JAMII TENGERU
 


TANGAZO LA MAHAFALI YA SITA YA TAASISI
MKUU WA TAASISI YA MAENDELEO YA JAMII TENGERU, ANAWAALIKA WAHITIMU NA WADAU WOTE WA MAENDELEO YA JAMII KWENYE MAHAFALI YA SITA (6) MWAKA 2015/2016 KATIKA KOZI ZA STASHAHADA YA UZAMILI YA MAENDELEO YA JAMII, SHAHADA ZA MAENDELEO YA JAMII –USIMAMIZI WA PROGRAMU ZA MAENDELEO YA JAMII, UPANGAJI NA UENDESHAJI WA MIRADI, JINSIA NA MAENDELEO NA MAHAFALI YA KWANZA YA ASTASHAHADA YATAKAYOFANYIKA TAREHE 25/11/2016 SIKU YA IJUMAA KATIKA VIWANJA VYA TAASISI KUANZIA SAA NNE (4) ASUBUHI.
MGENI RASMI ATAKUWA NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA WATOTO NA WAZEE MH.DR. HAMISI KIGWANGALLA (Mb)

MAZOEZI YA SHEREHE YA MAHAFALI YATAFANYIKA TAREHE 24/11/2016 KUANZIA SAA 9 ALASIRI. AMBAYE HATAHUDHURIA MAZOEZI HAYO, HATAHUDHURISHWA.

WAHITIMU WOTE WATAKAOHUDHURIA MAHAFALI HAYA WANATAKIWA KUTHIBITISHA USHIRIKI WAO KWA KAIMU MSAJILI, KWA SIMU NAMBA 0784315619/ 0762678000 BARUA PEPE: almasi.juma@cdti.ac.tz 

MAJOHO YANAPATIKANA CHUONI KWA TZSHS 30,000/. MALIPO YAFANYIKE BENKI YA NMB AKAUNTI NO: 4081100060 NA UTOAJI WA MAJOHO UTAANZA TAREHE 21/11/2016 HADI 24/11/2016. MHITIMU ATATAKIWA KUJAZA MKATABA WA UKODISHAJI WA JOHO.TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA MKUU WA TAASISI

About Woinde Shizza

Mwandishi , Mjasiriamali na Mbunifu wa Mavazi. Email : woindeshizza@gmail.com , Instagram: woindeshizzablog.