Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akiongea na waendesha boda boda wa jiji la Arusha ambapo alisema kuwa nimefanya kikao na vijana wa Bodaboda Jiji la Arusha. Tunawaandalia
utaratibu mzuri wa kujikwamua kiuchumi. Tumewatafutia pikipiki 200(zenye
thamani ya Million 400 ) ambazo tutawagawia bila riba wala dhamana.
Badala ya kupeleka pesa kwa tajiri watapelekea kwenye mfuko wao na
ikitimia pesa ya pikipiki , hiyo inakuwa Mali yake na tuna
nunua pikipiki nyingine na kumpa kijana mwingine. Pia tumezikatia BIMA
kubwa na Mbunge wa Viti maalum (Mhe Catherine Magige) atawalipia bima ya
afya kaya zote 200. Pia tutawapatia mafunzo. Uongozi unao acha alama. |
-
0 Comments
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia