Ticker

6/recent/ticker-posts

AFP: DK SHEIN AMEWAACHA SOLEMBA WAROHO WA MAFUTA ZANZIBAR


Image result for MAFUTA ZANZIBAR
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

Chama cha Wakukima Tanzania (AFP) kimesema Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohaned
Shein hajavunja katiba wala sheria katika kusaini mswada wa uchimbaji
mafuta kuwa sheria na kusema wanasiasa wanaoeneza maneno hayo wana majuto
baada ya kufungwa goli la kisigino.

Pia chama hicho kimesifu msimamo wa Rais huyo kwa kufanikiwa jina lake
kuliingiza katika kurasa mpya za historia kwa uamuzi wake wa kusaini sheria
ya utafutaji na uchimbaji mafuta na gesi asilia visiwani humu.

Mwenyekiti wa AFP Said Soud Said alitoa msimamo huo  katika ofisi ya
jimbo ya Chama hicho  huko Chukwani nje kidogo ya mji wa Unguja na
kusisitiza mafuta yatakapoanza kutafutwa na kuchimbwa maisha ya watu
zanzibar kiuchumi yatatononeka na kubadilika.

Soud alisema Rais amesaini Mswada wa sheria ya utafutaji na uchimbaji wa
mafuta na gesi asilia huku akionyesha msisitizo na kujiamini kwamba  Katiba
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haikuvunjwa na suala hilo lina baraka
zote  kisheria .

" sheria ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia wa mwaka 2016
taratibu zote zimefuatwa wakati wa mchakato wa kutunga kwa sheria,wanasiasa
waonapiga mayowe wameachwa solemba na kufungwa goli la kisigino "alieleza
Soud

Alisema  masharti ya kifungu cha nne Sheria ya Mafuta na Gesi Asilia 2015
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kinataja  shughuli za uendeshaji wa
Mafuta na Gesi Asilia utafanywa Zanzibar kwa kusimamia na kuendeshwa
kitaasisi kwa mujibu wa Sheria za Zanzibar sibvinginevyo hivyo hakuna
kilichokiukwa

“nawaasa Wazanzibari wenzangu tusikubali kugawanywa  na wanasiasa waroho wa
madaraka  waliokuwa na ndoto ya kuhodhi hisa na  visima vya mafuta ,
wangepata madaraka na mpango wa kukomba  mafuta wangefumba midomo yao ,
wanapaza sauti baaada ya kuzidiwa kete ” Alisisitiza Rais Dk. Shein.

Mwenyekiti huyo wa AFP aliwataka wananchi wasikubali kuyumbishwa na wala
wasibabaishwe na watu wasioitakia mema Zanzibar na kwamba sheria hiyo
itafungua fursa za kimaendeleo kwa kampuni nyingi  kujitokeza kuanza kazi
ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asili Visiwani humo .

Alisema wapo baadhi ya wanasiasa wa Zanzibari hawapendi kuwaona wenzao
wakifanya jambo jema na kutaka kila kitu waonekane wao ndiyo ree na wajuzi
wa mambo au wenye akili na maarifa hivyo wanapoona wengine wanaleta maajabu
kimaendeleo, hupotosha ukwell na kuudanganya umma kwa maslahi yao.

Aidha kiongozi huyo wa AFP ambaye pia ni Waziri Asiye na Wizara Maalum SMZ
, alisema Rais Dk Shein ana dhamira njema , mipango na malengo ya
kuwaendeleza kiuchumi wananchi wa Unguja na Pemba tofauti na wengine ambao
hupigia maslahi ya walioponduliwa.

"Tokea mwaka 1963 Zanzibar kulionekana dalili za kuwepo mafuta unguja na
Pemba, marais wote hawakushughulikia suala hilo, Dk Shein sasa amethubutu
na atafanikiwa kuiletea neema Zanzibar hata baaada ya kuondoka kwake
madaraka "alieleza Soud

Hata hivyo Soud aliwataka wazanzibari kuwa makini , watulivu, wenye subira
na matumaini kwasababu utafutaji na uchimbaji wa mafuta aghalab huandamwa
na fitna, majungu na mgawanyiko kama ilivyotokea huko Delta nchini Nigeria

Pia alisema pamoja na kuwepo kwa matumaini ya kupatikana mafuta, amehimiza
kuendelezwa kwa kilimo cha karafuu na minazi kwani mazao hayo alidao
yataisaidia sana Zanzibar kiuchumi na watu wake pamoja na kilimo cha
matunda na manukato .

Rais Dk Shein aliwaeleza waandishi wa habari kuwa Septemba mwaka 2016, Sera
ya Mafuta na Gesi  ilisharidhiwa na Baraza la Mapinduzi na Baraza la
Wawakilishi la Zanzibar lilipitisha rasmi Sheria ya Utafutaji na Uchimbaji
wa Mafuta ya Zanzibar ambayo sass ameitia saini kuwa sheria na kuanza
kutumika.

Post a Comment

0 Comments