Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Dkt. Tito Mwinuka, (kushoto), akipokea kikombe (tuzo), kutoka kwa Mwakilishi wa Wahandisi wanawake kutoka Shirika hilo, Mhandisi Rosamystica Lutenganya, katika hafla fupi iliyofanyika makao makuu ya Shirika hilo jijini Dar es Salaam Agosti 25, 2017. Wahandisi wanawake wa TANESCO walikabidhiwa tuzo hiyo na Makamu wa Rais, baada ya kuibuka wa kwanza kwenye kongamano na maonesho linalowakutanisha wahandisi wanawake kutoka sekta mbalimbali hapa nchini lijulikanalo kama "Tanzania Women Engineers Convention and Exhibition-TW=AWECE". Wahandisi hao walionesha umahiri mkubwa jinsi wanavyoweza kutumia teknolojia ya kisasa katika usimamizi wa miundombinu ya usambazaji umeme (Distribution Control Centre) inayotumika kuboresha huduma.
NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
KAIMU
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Dkt. Tito Mwinuka, (pichani),
amewataka Wahandisi Wanawake wa Shirika hilo, kutembelea mashuleni ili
kuwahamasisha (Motivate), wanafunzi wa kike ili wapende kujisomea masomo ya
sayansi na Hisabati na hatimaye baadaye waje kushika nafasi kama walizo nazo
wao.
Dkt.
Mwinuka ameyasema hayo makao makuu ya TANESCO jijini Dar es Salaam, wakati
akiwapongeza Wahandisi wanawake wa Shirika hilo, baada ya kupewa tuzo na Makamu
nwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, kwa
kuibuka wakwanza kwenye Kongamano la Wahandisi wanawake Tanzania “Tanzania Women
Engineers Convention and Exhibition, (TAWECE), ambalo huenda sambamba na
maonesho ya shughuli za kihandisi lililofanyika hivi karibuni jijini Dar es
Salaam.
“Niwapongeze
sana kwa kuibuka washindi wa kwanza kwenye maonesho hayo, lakini niwaase,
mpatapo nafasi mtembelee mashuleni ili muwahamasishe wanafunzi wasichana
kupenda kusoma masomo ya sayansi na hisabati, na kwa kupitia kwenu, wanaweza
kujitokeza wasichana wengi kupenda masomo hayo na hivyo baadaye kufanya kazi za
kihandisi kama nyinyi.” Alisema Dkt. Mwinuka.
Dkt.
Mwinuka alisema, tuzo hiyo ni heshima kubwa kwa Shirika kwani inajenga picha
(image) nzuri mbele ya jamii kuonyesha juhudi zetu za kuwahudumia wateja wetu.
Alisema.
Akizungumza
kwa niaba ya wenzake kwenye hafla hiyo fupi, Mhandisi Rosamystica Lutenganya,
alisema Wahandisi wanawake kutoka TANESCO, walionyesha umahiri wao katika
kuelezea teknolojia ya usimamizi wa miundombinu ya usambazaji umeme
(Distribution Control Centre), inayotumia kuboresha huduma wanazozitoa katika
jamii.
“Lakini
pia si hivyo tu, tulionyesha uboreshaji wa huduma tunazozitoa kwa wateja kwa
kutumia teknolojia ya kisasa kupitia mfumo wa fiber ambao upitishaji taarifa
mbalimbali kama vile mawasiliano na picha na hii inawezesha mfumo kuliona
tatizo la mteja mara tu linapotokea na kuwezesha TANESCO kuchukua hatua haraka
bila mteja kupata usumbufu.” Alisema Mhandisi Lutenganya.
Katika
Kongamano hilo la mwaka huu lililofanyika Julai 28, (2017), kulikuwa na makundi
matatu ya washiriki, ambayo ni shule za Sekondari, taasisi za elimu ya juu na
mashirika ya umma ambapo waandaaji waliangalia uandaaji, uelewa wa washiriki
pamoja na teknolojia ilivyotumika.
TANESCO
ina wahandisi wanawake 55, na kuifanya taasisi ya kwanza nchini kuwa na idadi
kubwa na wahandisi wanawake.
Naye
Naibu Mkurugenzi Mtendaji waTANESCO (anayeshughulikia usambazaji na huduma kwa
wateja), Mhandisi Joyce Ngahyoma, alisema ni wajibu wa wanawake kujiamini
katika utekelezaji wa majukumu yao na kuachana na dhana ya woga.
“Fanyeni
kazi kwa bidii na maarifa, na niwaambie, utendaji kazi wako ndio utamvutia MD
afikie uamuzi wa kukupandisha cheo na sio jambo linguine lolote lile, mimi nitastaafu
hivi karibuni, ninawaeleza haya kwavile ninajua umuhimu wa kujituma katika kazi
na kujiamini.” Alisema Mhandisi Ngahyoma.Alionyesha
kufurahishwa kwake, na angependa idadi ya wanawake viongozi katika Shirika hilo
inaongezeka na kufikia sio asilimia 50 tu bali asilimia 75.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji waTANESCO (anayeshughulikia usambazaji na huduma kwa wateja), Mhandisi Joyce Ngahyoma, akiwa na Dkt. Mwinuka wakati akionyesha tuzo hiyo. |
Dkt. Mwinuka, akiwapongeza baadhi ya wahandisi hao.
Dkt. Mwinuka akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji waTANESCO (anayeshughulikia usambazaji na huduma kwa wateja), Mhandisi Joyce Ngahyoma, akitoa nasaha zake. |
Mwakilishi wa Wahandisi wanawake kutoka Shirika hilo, Mhandisi Rosamystica Lutenganya, akizungumza.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji waTANESCO (anayeshughulikia usambazaji na huduma kwa
wateja), Mhandisi Joyce Ngahyoma, akitoa nasaha zake.
Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji, akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji, akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Picha ya pamoja.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia