Diwani
wa kata ya Nkoanekoli Wilson
Nanyaro akifafanua jambo katika baraza
la madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Meru
Diwani
kata ya Malula na Makamu Mwenyekiti wa
Baraza la Halmashauri ya Wilaya Meru Nelson Mafie akizungumza katika kikao cha
Baraza hilo
Wananchi wa Vijiji na Kata
zinazopakana na hifadhi ya taifa ya Arusha (ANAPA) wameiomba serikali kupitia
kitengo cha Maliasili kuwalipa inayotokana na uharibifu wa mazao ya
chakula unaofanywa na wanyamapori.
Wakiwasilisha malalamiko kwenye
Kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Meru ,
Diwani wa kata ya Nkoanekoli Wilson Nanyaro alisema kuwa
jumla ya ekari 6 za mazao zimeharibiwa na wanyamapori hivyo wameiomba idara ya
Maliasili ili kunusuru kaya 12 na uhaba wa chakula.
Nanyaro alisema kuwa katika kipindi
hiki cha mavuno wananchi hao wamepata mazao machache sana kutokana na mazao yao
kuliwa na nyani ambao hutoka hifadhi hiyo ya taifa.
Diwani viti Maalumu kata ya Embaseny
Agness Lambo Alisema kuwa wamekua wakitoa taarifa kwa idara hiyo ila
wakichelewa kuzifanyia kazi kwa muda muafaka hivyo kusababisha maumivu ya
kiuchumi kwa wananchi ambao hutegemea kilimo kujikwamua kimaisha.
“Wananchi waliokubwa na adha hii
wanaishi umbali mrefu kutoka katika hifadhi ya Arusha tumekua tukitoa taarifa
ila Maafisa wa Maliasili wamekua wakichelewa mara kwa mara hivyo kusababisha
wananchi kutokupata haki stahiki” Alisema Lambo
Afisa Maliasili Halmashauri ya
Wilaya ya Meru Bernad Saruni amekiri kuwepo kwa tattizo hilo na tayari wameanza
kuwalipa fidia wananchi wa kijiji cha Leguruki,Ngarinanyuki fedha ambazo
ni kifuta machozi baada ya uharibifu huo kutokea.
Hata hivyo amewataka Wananchi
kuzingatia vigezo muhimu ili kufidiwa ikiwemo kufanya shughuli zao umbali wa
mita 500 kutoka katika mpaka wa hifadhi ya taifa ya Arusha na pia kutumia njia
za asili kuyalinda mazao yao yasiharibiwe na wanyama…
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia