Na Tiganya Vincent.
SERIKALI
Mkoa wa Tabora imeagiza kutafutwa na kuchukiwa hatua kali na kupata
maelezo ya watu waliohusika na uchomaji moto katika maeneo ya Chuo cha
Ardhi Tabora na kusababisha uharibifu mkubwa wa mistu asili na miti
iliyokuwa imepandwa katika eneo hilo kama hatua za uhifadhi wa
mazingira.
Kauli
hiyo imetolewa jana mjini hapa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri
baada ya kukuta eneo la Chuo hicho likiwa limeungua na moto wakati wa
ziara ya ya kukagua vitalu vya kuoteshea miti ikiwa ni maandilizi ya
zoezi la upandaji wa miti.
Alisema
kuwa haiwezekani wananchi wanajitoa kwa moyo kupanda miti katika
kampeni inayoendelea kisha watu wachache wanaamua kuua miti na kuharibu
mazingira.
Mwanri
aliongeza kuwa inasikitisha kuona hata sehemu za Taasisi za umma kama
hiyo zinaacha moto unaunguza miti na wakufunzi wapo, wanachuo wapo bila
kuchukua hatua ya kuuzima na kuwasaka waliohusika.
Alisema
kitendo kinaonyesha jinsi wao nao wanahusika kwa namna moja au nyingine
katika kuchangia uharibifu ulifanyika katika Chuo chako.
Kufuatia
kitecho hicho Mkuu wa Mkoa alimwagiza Afisa Mazingira wa Manispaa ya
Tabora kwenda kwa Mkuu wa Chuo kupata maelezo nini kilitokea na hatua
zilizochukuliwa kwa wahusika na kama hawachukua hatua kwa wahusika basi
Sheria za Mazingira zichukue mkondo wake.
Aliongeza
kuwa pamoja na hatua hiyo zitakazochuliwa aliagiza uongozi wa Chuo
hicho kuhakikisha wanarudishia miti yote iliungua mapema iwezekanavyo.“Nimesikitishwa
na kitengo nilichokiona katika eneo la Chuo cha kuchoma moto na
kuunguza miti ,kiwa kwa watu wasomi ambao wanatakiwa wawe mfano wa
utunzaji wa mazingira wao ndio wanakuwa wa kwanza kuharibu mazingira kwa
kuchoma moto…nimesikitishwa sana” alisema Mkuu huyo wa Mkoa.
Naye
Afisa Mazingira wa Manispaa ya Tabora William Mpangala alisema hadi
hivi sasa Ofisi yake imekwishakamata watu 27 kwa makosa ya uchomaji moto
ovyo na kuwapiga faini ya kuanzia 50,000/-
Alisema
kuwa viongozi wa Taasisi wafahamu kuwa kunapotokea moto katika maeneo
yao wakishindwa kuwakamata wahalifu wao watawajibika kulipa faini ya
uharibifu wa mazingira ya kuanzia shilingi 500,000/-.
Utamaduni
wa uchomaji moto ovyo katika Mkoa wa Tabora unaoenekana kama kama jambo
la kawaida wengine wakitaka malisho mapya ya mifugo na mengine wakati
wa kuandaa mashamba na wakati wa kulina asali.
Jambo
hilo limekuwa likimuumiza kichwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora wakati mwingine
kulizamika kuamuka usiku kuwavizia watu wanaowasha moto ovyo.
Wakati
huo huo Mkuu wa Mkoa wa Tabora ameziagiza Halmashauri zote mkoani
kuhakikisha vitalu vya miti waliyotayarisha kwa ajili awamu ya pili ya
upandaji mkoani hapa inayomiti ya kutosha kwa kadri walivyokubaliana.
Alisema
kuwa Manispaa ya Tabora inapaswa kuhakikisha imeotosha miche 500,000,
Nzega Mji na Wilaya miche 500,000 na nyingine zilizobaki 250,000 kila
moja.
Mwanri
idadi hiyo ni nje ya ile ambapo kila mkazi wa Tabora atakiwa kupanda au
kupandiwa na mzazi wake kama ni mtoto miti miwili kila mmoja.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia