Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson
(mwenye baiskeli wa pili kulia) akiwa na viongozi wa Mkoa na baadhi ya
Wabunge wa Mkoa wa Simiyu na Viti Maalum kutoka nje ya Mkoa kwa ajili ya
kufungua mashindano ya baiskeli yaliyofanyika Mjini Bariadi.
Na Stella Kalinga, Simiyu
Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia
Ackson amefungua Mashindano ya Mbio za Baiskeli na Ngoma za Asili Mjini
Bariadi(Simiyu Jambo Festival) ambayo yamehudhuriwa na Maelfu ya
Wananchi wa Mkoa wa Simiyu. Mashindano hayo ya mbio za baiskeli
yamehusisha kilometa 200 wanaume, kilomita 80 wanawake ambapo pia
walemavu waliweza kushindania katika umbali wa kilomita tano.
Akizungumza
baada ya kufungua mashindano hayo Dkt.Tulia pamoja na kuupongeza Mkoa
wa Simiyu kuandaa mashindano hayo amesema, ipo michezo nchini haijapewa
kipaumbele lakini ikitumiwa vizuri inaweza kutoa ajira ukiwemo mchezo wa
mbio za baiskeli; ambapo ametoa wito kwa viongozi wa mikoa mingine pia
kuwekeza katika michezo mbalimbali ili kuwasaidia wananchi kupata
kipato.
“Lililofanyika
Simiyu ni jambo jema sasa watu watakuwa wanajua kuwa wakijifua vizuri
kwenye baiskeli na ngoma za jadi wanakuja kushiriki mashindano ya
Baiskeli Simiyu, nitoe wito kwa viongozi wengine kufikiria mambo mengine
yanayoweza kuwasaidia wananchi katika maeneo yao kupata ajira na
kujipatia kipato” alisema.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amesema mkakati wa mkoa huo ni
kurasimisha tamaduni zote za Mkoa wa Simiyu na kuhusianisha na shughuli
za Utalii ndani ya mkoa huo. “Position(Nafasi) ya Mkoa wa Simiyu kwenye
nchi ni kukuza tamaduni na sanaa zetu kama moja ya eneo
litakalotuunganisha na sekta ya Utalii, tumezungukwa na mapori ya akiba
na mbuga za wanyama, tungehitaji watalii wanapokuja kwenye maeneo hayo
wapate ladha ya tofauti kiwemo utamaduni wa Mtanzania”.
Mtaka
ameongeza kuwa wasanii wote watatambuliwa na baadae kujengewa uwezo
kupitia watalaam wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(Kitivo cha sanaa),Chuo
cha Sanaa Bagamoyo na vyuo vya michezo ili waweze kufanya kazi zao
kibiashara na kuimarisha uchumi wao.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Food Products,Mhe.Salum
Khamis ambaye ndio Mdhamini wa mashindano ya Baiskeli na ngoma za Asili
(Simiyu Jambo Festival) amesema ataendelea kudhamini mashindano kama
hayo Mkoani Simiyu ili kuwaweseha wananchi kuinua kipato kupitia vipaji
vyao. Naye mshindi wa kwanza mbio za kilometa 80 (wanawake) Raulensia
Luzuba kutoka Mwanza ameomba mashirika na makampuni mbalimbali
kuwadhamini ili waweze kujengewa uwezo na kuandaliwa kushiriki katika
mashindano ya Kimataifa.
Masunga
Duba mshindi wa mbio za kilometa 200(wanaume)kutoka Simiyu amesema
pamoja na wafadhili kudhamini mashindano ameomba pia wawasaidie
wachezaji kupata baiskeli za kisasa zitakazowasaidia kwenda kwa kasi
inayotakiwa.
Mashindano
ya baiskeli Mkoani Simiyu yameshirikisha wachezaji kutoka mikoa ya
Simiyu, Mwanza, Shinyanga,Arusha na Mbeya ambapo ushindi kwa upande wa
wanaume umechukuliwa na Hamisi Hussein(Arusha) ambaye amejishindia
pikipiki, wa pili ni Masunga Duba(Simiyu) kitita cha shilingi
1,000,000/= wa tatu Richard Laizer .shilingi 500,000/= na zawadi
nyingine zimetolewa kwa mshindi wa nne mpaka wa 15.
Kwa
upande wa wanawake mshindi wa kwanza Raulensia Luzuba kutoka Mwanza
amejipatia shilingi 500,000/=, mshindi wa pili Tatu Malulu(Mwanza)
shilingi 400,000/= na wa tatu ni Vumilia Mwinamila(Simiyu) shilingi
300,000/= na zawadi nyingine zimetolewa kwa mshindi wa nne mpaka wa 10.
Walemavu mshindi wa kwanza Emmanuel Mtemi amejipatia shilingi 200,000/=
wa pili Masunga Sendama shilingi 150,000/= na wa tatu Saguda Sospeter
shilingi 100,000/=wote kutoka mkoa wa Simiyu na zawadi nyingine
zimetolewa kwa mshindi wa nne na wa tano.
Mshindi wa tatu mbio za baiskeli kilometa 80(wanawake), Vumilia Mwinakila kutoka Mkoa
wa Simiyu akicheza wimbo wa Kisukuma pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka na
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson baada ya kupokea kitita cha
shilingi laki tatu.
mshindi wa kwanza kilometa 200 (wanaume), Hamisi Hussein kutoka Arusha akipanda
kwenye pikipiki yake aliyokabidhiwa baada ya kuibuka mshindi dhidi ya wenzake katika mashindano ya
Baiskeli yaliyofanyika Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Rais wa Chama cha Baiskeli Taifa, Godfrey Mhagama akimkabidhi mshindi wa kwanza katika
mbio za kilometa 10 (walemavu) katika mashindano ya Baiskeli na ngoma za asili (Simiyu Jambo Festival)
yaliyofanyika Mjini Bariadi Simiyu.
Mkurugenzi Kampuni ya Jambo Food Products, Mhe.Salum Hamis ambaye ndio mdhamini wa
mashindano ya baiskeli na ngoma za asili akimkabidhi Mshindi wa kwanza mbio za Kilometa 80 (wanawake)
Raulensia Luzuba kutoka mkoani Mwanza zawadi ya shilingi laki tano taslimu.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson akiwa katika
picha ya pamoja na washindi watatu wa mbio za Kilometa 80(wanawake) na viongozi wa Mkoa wa Simiyu na
baadhi kutoka nje ya mkoa wa Simiyu, mara baada ya kumalizika kwa mashindano ya baiskeli na Ngoma za
Asili(Simiyu Jambo Festival) Mjini Bariadi.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson (wa pili
kushoto) akimkabidhi ufunguo wa pikipiki mshindi wa kwanza kilometa 200 (wanaume), Hamisi Hussein
kutoka Arusha katika mashindano ya Baiskeli yaliyofanyika Mjini Bariadi (kulia) ni Mkurugenzi Kampuni ya
Jambo Food Products ambayo ni mdhamini, Mhe.Salum Khamis akimpongeza Mshindi huyo
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson akiwa katika
picha ya pamoja na washindi watatu wa mbio za Kilometa 10 (walemavu) na viongozi wa Mkoa wa Simiyu na
baadhi kutoka nje ya mkoa wa Simiyu, mara baada ya kumalizika kwa mashindano ya baiskeli na Ngoma za
Asili(Simiyu Jambo Festival) Mjini Bariadi.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson akimkabidhi
ufunguo wa pikipiki mshindi wa kwanza (wanaume) katika mashindano ya Baiskeli yaliyofanyika Mjini Bariadi
kilometa 200, Hamisi Hussein kutoka Arusha.
Washiriki wa mashindano ya mbio za Baiskeli kilometa 200(wanaume) wakiendelea kuchuana
vikali kushindania pikipiki na fedha taslimu.
Wa pili kutoka kushoto Katibu Tawala mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini, Mbunge wa
Busega, Mhe.Raphael Chegeni , Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia
Ackson wakiwa wamembeba nyoka wa kikundi cha wasanii wa ngoma ya asili ya Kisukuma.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia