Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM)
Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akizungumza na Viongozi
Mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake Mara baada ya kuzuru
katika Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba.
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM)
Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akisaini kitabu cha wageni Mara baada ya kuzuru
katika Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba.
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM)
Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akionyesha ilani ilani ya CCM mwaka 2015-2020 na maelekezo ya namna ya utekelezaji wakati akizungumza na Viongozi
Mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake Mara baada ya kuzuru
katika Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba Ndg Abdallah
Rashid Ali akielezea namna Ofisi ya Mkuu wa Wilaya inavyotekeleza ilani
ya CCM mbele ya Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM)
Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) Mara baada ya kuzuru
katika Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba.
Na Mathias Canal, Kusini Pemba
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) kwa kauli moja Umewataka
watumishi wa Umma kote nchini Kutekeleza ilani ya Uchaguzi ya CCM ya
Mwaka 2015-2020 kwa kutenganisha Siasa na shughuli za maendeleo.
Kauli hiyo imetolewa leo Agosti 15, 2017 na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM
Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) alipokuwa akizungumza na Viongozi
Mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake Mara baada ya kuzuru
katika Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba.
Shaka ametilia mkazo zaidi kwa kuwataka Watumishi wa Serikali
kutenganisha siasa na Majukumu ya kazi kwa Wananchi ili kuwaletea
maendeleo pasina kuwabagua kwa dini, kabila ama utofauti wa itikadi za
vyama vya kisiasa.
Alisema kuwa litakuwa Jambo la aibu tena
lisilovumilika kwa Viongozi wa Umma kushughulika na Mambo ya siasa kwani
hizo Ni kazi za vyama vya siasa ambavyo hata vyama vya siasa vina
mipaka katika kufanya siasa.
Shaka Alisema kuwa watumishi wa Umma
wamepewa dhamana kubwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe
Dkt John Pombe Magufuli hivyo Ni matarajio ya Chama Cha Mapinduzi CCM na
Serikali, watumishi wote Kusimamia na kuwajibika ili Kutekeleza imara
ilani kwa utayari.
Alisema kuwa ilani ya CCM imeielekeza Serikali
kufanya Mambo mengi ya Maendeleo ambayo kwa asilimia kubwa tayari
yameanza kutekelezwa kwa usimamizi mzuri wa Rais Magufuli.
Alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ipo chini ya CCM hivyo
kila kiongozi aliyeajiriwa na Serikali Ana jukumu moja kubwa la
Kutekeleza ilani kwa umakini mkubwa kwa maslahi mapana ya Taifa.
"Kama kuna mtumishi asiyefanya hivyo basi ni wazi kuwa hastahili kuendelea kuwa kwenye nafasi yake"
"Tunakuwa na mipango mingi lakini utekelezaji wake unasuasua kwa
kisingizio Cha bajeti ndugu zangu ifike Wakati tuwe na bajeti
inayotekelezwa na itekelezwe kwa umakini, uangalifu na weledi Mkubwa"
Alisema Shaka
Alisema kuwa watumishi wa serikalini wanapaswa
kubainisha vyema Mipango ya muda mfupi na muda mrefu kwa manufaa ya
Wananchi pasina kuwabagua zaidi ni kukubali kuwa wawajibikaji wazuri.
Katika Hatua nyingine UVCCM Taifa imempongeza Rais wa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar Mhe Dkt Ali Mohed Shein kwa maendeleo endelevu
aliyoyafanya katika kipindi Chake tangu amekuwa Rais wa Zanzibar kwa
kuimarisha Huduma za uwanja wa Ndege, uchumi wa Pemba umeimarika, fursa
za uwekezaji sio Kama kipindi kilichopita.
Umoja huo umesisitiza
kuwa Ni vyema wasaidizi wa Rais kumsaidia kwa vitendo sio maneno kwani
Ni Lazima Viongozi kuwa na uthubutu na uwajibikaji.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia