NITAHESHIMU MIAKA 10 YA URAIS KWA MUJIBU WA KATIBA SITAONGEZA MUDA :RAIS MAGUFULI

Mbunge: Rais Magufuli Aongezewe Muda wa Kukaa Madarakani
KUTOKA TANGA, KOROGWE: Taarifa zinaeleza kuwa Mbunge Stephen Ngonyani(Prof. Maji Marefu) amesema kuwa Rais Magufuli anapaswa kuongezewa muda wa kukaa madarakani ili akamilishe mambo mengi. Amesema Rais Magufuli anamaliza ziara yake ya siku ya tano ambapo leo atakuwa wilayani Korogwe kufungua stendi mpya ya mabasi.

Rais John Pombe Magufuli akiwa Korogwe mkoani Tanga amesema hayuko tayari kuendelea kuongoza baada ya miaka 10. Amesema ataheshimu Katiba ambayo imeweka ukomo wa miaka 10 na si vinginevyo.Rais ametoa kauli hiyo Leo baada ya Mbunge wa Korogwe Vijijini, Steven Ngonyani (Prof. Maji Marefu) kusema Rais anastahili kuongezwa muda ilia afanye mambo mengi zaidi. Kutokana na kauli ya Rais ya Leo, ameondoa taarifa za mitaani na kwenye baadhi ya vyombo vya habari kwamba Rais Magufuli anaweza kuongeza muda wa kuaa madarakani. 

About Woinde Shizza

Mwandishi , Mjasiriamali na Mbunifu wa Mavazi. Email : woindeshizza@gmail.com , Instagram: woindeshizzablog.