Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla,amezuia likizo na
safari zote kwa Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri na Wakuu wa
Idara za Mkoa huo, baada ya kushindwa kuandaa mpango kazi wa kutekeleza
dhanaya Viwanda, ambao ni kipaumbele cha serikali ya awamu ya tano.
Alitoa agizo hilo jana Wilayani Rungwe,wakati wa kikao cha
Baraza la Madiwani cha kupitia na kutoa majibu ya hoja za Mkaguzi Mkuu
na Mdhibiti wa hesabu za serikali (CAG).
Makalla alifikia hatua hiyo, kutokana na
makubaliayaliyofikiwa na viongozi hao June 2 mwaka huu,ambapo walipeana
majukumu ya namna Mkoa huo utakavyotekeleza uanzishwaji wa viwanda.
Mkuu
huyo wa Mkoa alisema, katika hali ya kushangaza hadi kufikia sasa
hakuna Halmashauri hata moja ambayo imendaa mpango kazi wa uanzishwaji
wa viwanda.
“Kuanzia sasa hakuna, Mkuu wa Wilaya,Mkurugenzi au Mkuu wa
idara kutoka nje ya Mkoa, labda kwa wale wenye matatizo kama kuumwa na
mialiko yote ya semina sasa isomeni, weka pembeni…maana ukiuliza
watendaji utasikia tuko mbioni, sasa nimeona safari za kufuata mialiko
Dodoma ziwe mwisho. ” alifafanua Makalla.
Aidha, Makalla aliwataka wakurugenzi wote wa Halmashauri
saba za Mkoa huo, wakishirikiana na Madiwani kusimamia kwa umakini
vyanzo vya mapato ili kuinua mapato na kuepukana na utegemezi kutoka
serikali Kuu.
Alisema kwa mujibu wa taarifa hiyo ya CAG , Halmashauri
hizo za Mkoa wa Mbeya zinajitegemea kwa asilimia 6.6 tu, huku
zikitegemea ngvu ya serikali kuu kwa asilimia 93.6, kinyume na agizo la
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, aliyeagiza Halmashauri zote nchini
kukusanya asilimia 80 kutoka vyanzo vyake vya ndani.
Akizungumza nje ya kikao hicho, Diwani wa kata ya Kyimo,
Peter Makoye, alipongeza hatua iliyochukuliwa na Mkuu wa Mkoa akieleza
kuwa, limekuja kwa wakati muafaka kwa kuwa licha ya Rais, Dk. John
Magufuli kutoa muelekeo wake, bado baadhi ya watendaji wamekuwa
hawatekelezi
Naye Diwani wa kata ya Kawetele, Anyimike
Anganile, alionekana kushtushwa na taarifailiyotolewa mbele ya mkuu wa
Mkoa kuwa Wilaya ya Rungwe ina uhaba wa ardhi ya uwekezaji
“Uwezo wa kuwekeza katika viwanda kwa Rungwe ni mkubwa kwa
kuwa, kuna maeneo mengi Mfano kata za Ilima, Kisondela na Ibigi ambako
kuna mashamba ya halmashauri, lakini shida imekuwa ni dhamira ya
viongozi kutaka kuwekwa mjini” alisema Anganile.
Mkoa wa Mbeya ulikuwa ni miongoni mwa mikoa iliyokuwa na
idadi kubwa ya viwanda, lakini vilibinafsishwa kwa wakezaji na kushindwa
kuviendesha,.
Miongoni mwa viwanda hivyo vilivyobinafsishwa na
kushindwa kuendelea na uendeshajini ni kiwanda cha nguo cha Mbeya
Tixtile, kiwanda cha kutengeneza zana za kilimo (ZZK), kiwanda cha
Sabuni cha Hisoap, pamoja na kile cha nyama cha Tanganyika Packers.