17 of 3,670 DR. MENGI ATAKA EAC KUTUMIA UTAJIRI WAKE KUTENGENEZA MABILIONEA
MWENYEKITI
wa Taasisi ya sekta binafsi nchini (TPSF) Dr. Reginald Mengi amezitaka
Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kushirikiana katika kutumia utajiri
wake mkubwa wa raslimali kunufaika kiuchumi.
Ushirikiano
huo ni pamoja na kuzindeleza raslimali hizo na kutumia nembo moja ya
kibiashara ili kuzalisha mabilionea wakubwa duniani.
Mwenyekiti
huyo alisema hayo katika mkutano wa Taasisi za Sekta Binafsi za
Tanzania na Kenya zilizokutana jijini Dar es salaam kujadili kwa pamoja
namna ya kuondoa vikwazo vya kufanya biashara baina ya wafanyabiashara
wa nchi hizo mbili.
- Mwenyekiti wa Taasisi ya sekta binafsi nchini (TPSF) Dr. Reginald Mengi akizungumza wakati akifungua mkutano wa Taasisi za Sekta Binafsi za Tanzania na Kenya zilizokutana jijini Dar es salaam kujadili kwa pamoja namna ya kuondoa vikwazo vya kufanya biashara baina ya wafanyabiashara wa nchi hizo mbili uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Pamoja
na kutoa wito huo Dk Mengi pia amempongeza Rais wa Tanzania Dk John
Pombe Magufuli pamoja na serikali yake kwa kuwa mstari wa mbele
kuboresha ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na Kenya.
Aidha alisema dhamira yake ya kuigeuza Tanzania kuwa nchi ya viwanda itasaidia kuwakwamua Watanzania kutoka katika umaskini.
Katika
mazungumzo hayo ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Mwenyekiti wa Taasisi
ya Sekta Binafsi Tanzania –TPSF Dr Reginald Mengi na Ujumbe wa Kenya
umeongozwa na Gavana wa Taasisi ya Sekta Binafsi ya Kenya – KEPSA Bw.
George Owuor.
Akizungumza
katika mkutano huo Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF Bw. Godfrey Simbeye
amesema mkutano huo umeitishwa kutokana na kujitokeza vikwazo vya
kufanya biashara baina ya Wafanyabiashara wa Tanzania na Kenya, jambo
linalokwamisha malengo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya kujenga uchumi
unaoongozwa na sekta Binafsi.
Kwa
upande wake Kiongozi wa Ujumbe wa KEPSA Bw. George Owuor amesema
Wafanyabiashara wa Kenya wanapenda sana kushirikiana kibiashara na
wenzao wa Tanzania, na wangependa kuona vikwazo vinavyokwamisha
mahusiano ya kibiashara vinaondolewa.
- Gavana wa Taasisi ya Sekta Binafsi ya Kenya – KEPSA Bw. George Owuor akiwasilisha mada kuhusu kupunguza pengo la biashara kati ya Tanzania na Kenya na kutumia fursa zilizopo na kutanua biashara nje ya mipaka katika mkutano wa Taasisi za Sekta Binafsi za Tanzania na Kenya zilizokutana jijini Dar es salaam kujadili kwa pamoja namna ya kuondoa vikwazo vya kufanya biashara baina ya wafanyabiashara wa nchi hizo mbili uliofanyika jijini Dar es Salaam.
- Meneja anayeshughulikia Utafiti, Uchambuzi na Sera wa Taasisi ya Sekta Binafsi ya Kenya – KEPSA, Victor Ogalo (kushoto) akitoa mada kuhusu changamoto za kisera za Tanzania na Kenya katika mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam. Kulia walioketi ni Gavana wa Taasisi ya Sekta Binafsi ya Kenya – KEPSA Bw. George Owuor na Mwenyekiti wa Taasisi ya sekta binafsi nchini (TPSF) Dr. Reginald Mengi wakifuatilia kwa umakini mada hiyo.
- Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF Bw. Godfrey Simbeye (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Alaska Tanzania, Jennifer Bash wakifuatilia mada mbalimbali zikizokuwa zikiwasilishwa ukumbini hapo katika mkutano wa Taasisi za Sekta Binafsi za Tanzania na Kenya zilizokutana jijini Dar es salaam kujadili kwa pamoja namna ya kuondoa vikwazo vya kufanya biashara baina ya wafanyabiashara wa nchi hizo mbili uliofanyika jijini Dar es Salaam.
- Gavana wa Taasisi ya Sekta Binafsi ya Kenya – KEPSA Bw. George Owuor na mwenyeji wake Mwenyekiti wa Taasisi ya sekta binafsi nchini (TPSF) Dr. Reginald Mengi katika mkutano huo.
- Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF Bw. Godfrey Simbeye akijibu maswali kwa waandishi wa habari (hawapo pichani). Kulia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya sekta binafsi nchini (TPSF) Dr. Reginald Mengi.
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia