Mganga mkuu wa wilaya ya Arusha mjini Dokta Simoni
Chacha kwa kushirikiana timu yake ya mkoa imeanza kufanya operesheni maalum ya kukagua
maabara zote binafsi ili kubaini zile ambazo hazijasajiliwa na zilizokosa sifa ya
kutoa huduma katika jiji la Arusha.
Akizungumza na waandishi Dokta Chacha
amesema kuwa zoezi hilo limeanzia katika eneo la matejo kata ya Ngarenaro
ambapo wamekuta maabara ijulikanayo kwa jina la Sonogesha ambayo inatibu
wagonjwa kinyume cha taratibu.
Akizungumzia sifa za maabara zinazotakiwa Dokta Chacha
amesema kuwa lazima ziwe na watumishi wa
kutosha,cheti za usajili,vyumba vya kutosha kwa ajili ya huduma na maeneo ya
kutosha huku akisema zoezi hilo ni endelevu na hawatawaonea mtu huruma.
Hata hivyo maabara ambazo zimetembelewa zimegundulika kuwepo kwa mapungufu kama vibali kuisha muda
wake na kutoa huduma kinyume na taratibu utoaji wa dawa,kupima vipimo ambavyo hawakuruhusiwa
na kama vile Typhod na kukosa watumishi wenye sifa.
Vile vile maabara zilizopewa maelekezo na kupewa onyo ili waboreshe huduma ni
maabara ya TRUST health Laboratory service,Amani labaratory ,Arusha Jonior ,Global
Medicare, na morden klinic
Kwa upande wa wananchi wa jiji la Arusha wamepongeza
zoezi hilo ambalo wameanza huku wakibainisha kuwa maabara nyingi zimekuwa
zikitoza fedha nyingi kwa kutoa huduma ambazo hazilingani na fedha wanayotoa.