Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe William Tate Ole Nasha (Mb)akitoa maelekezo
kwa mtaalamu wa kilimo masoko uajasiriamali wa taasisi ya Nest of
God(kiota cha mungu ) Nelson Banda wakati alipotembelea banda lao
lililopo katika viwanja vya nane nane Themi jijini Arusha (picha na
Woinde Shizza,Arusha)
banda wizara ya maliasili na utalii lililopo katika viwanja vya nane nane Themi jijini Arusha
Afisa uhusiano wa hifathi ya Ngorongoro Nickson Nyange akiongea na waandishi wa habari katika banda lao ,ambapo alisema kuwa mamlaka ya hifadhi ya ngorongoro imetoa ofaya punguzo la garaza za kutembelea hifadhi hiyo na hii ni kwa wananchi wote wa Tanzania ambao ni watanzania kutembelea hifadhi ya ngorongoro kujionea vivutio mbalimbali vilivyopo katika hifadhi hiyo , ambapo alisema kuwa ofa hiyo itakuwa kwa muda wa siku tatu
Alisema kuwa punguzo hilo litawahusu wananchi ambao ni watanzania tu ambapo alisema watachangia kiasi cha shilingi elfu 50000 tu ambayo itakuwa ni kwa ajili ya usafiri chakula pamoja na viingilio vya hifadhi hiyo
Alisema kuwa safari zote zitaanzia asubuhi katika viwanja vya nane nane ambapo safari ndio itaanzia apo saa mbili na kurudi saa kumi
alitoa wito kwa watanzania wote kutumia fursa hiii kutembelea hifadhi ya ngorongoro kwani garama ambazo zimewekwa zipo chini
alisema malipo yote yanafanywa katika banda la ngorongoro ambalo lipo ndani ya viwanja vya nane nane njiro au katika ofisi zao zilizopo njini karibu na mnara wa saa
wananchi wakiangalia baadhi ya mazao yaliyolimwa kama shamba darasa katika viwanja vya nane nanejijini Arusha
Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe William Tate Ole Nasha (Mb)akiendelea kutembelea maonyesho ya nane nane jijini Arusha
mtaalamu wa kilimo masoko uajasiriamali wa taasisi ya Nest of
God(kiota cha mungu ) Nelson Banda wa tatu kulia akitoa maelezo
mbele ya naibu waziri wa kilimo mifugo na uvuvi mhe William Tate ole
Nasha wakati alipotembelea katika banda lao
wanangoma wa kundi la mjomba bandi wakiwa wanaburudisha wananchi ambao wamekuja kuuthuria maonyesho haya ya nane nane,kikundi hichi cha mjomba band kimeletwa kwa hisani ya Ngorongoro Concervation
wananchi wakiangalia bandi ya mjomba ikiwa inatumbuizi katika viwanja vya themi jijini Arusha
Serikali imeongeza uzalishaji katika
mazao makuu ya chakula hususani mahindi, mchele, mtama, uwele, na mikunde jambo
linalopelekea kujitosheleza kwa chakula kwa wastani wa asilimia 100.
Aidha, Uzalishaji mwingine umeongezeka
kwenye mazao ya jamii ya mizizi kama muhogo, ndizi, viazi vitamu na mviringo.
Hayo yamesemwa
na Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mhe. Wiliam Tate Ole Nasha (Mb)
wakati akizungumza na wakulima wadau wa kilimo Mifugo na Uvuvi na wananchi kwa
ujumla wakati wa uzinduzi wa sikukuu ya wakulima – nane nane, Maonesho yenye
kauli mbiu ya “Zalisha kwa Tija Mazao na
Bidhaa za Kilimo Mifugo na Uvuvi ili kufikia Uchumi wa Kati” yanayofanyika Kitaifa kwenye uwanja
wa maonesho ya kilimo wa Ngongo
Alisema kuwa Katika mwaka 2015/2016
Sekta ya Kilimo ilichangia asilimia 29.1 ya Pato la Taifa ikilinganishwa na
asilimia 29.0 mwaka 2014/2015. Mchango mkubwa katika Pato la Taifa ulitokana na
Sekta ya Kilimo, ikifuatiwa na Sekta nyingine za kiuchumi.
Mchango huo mkubwa ni Kwa kuwa
asilimia kubwa ya Watanzania wanashiriki katika shughuli za kilimo, hivyo
kilimo kinachangia kwa kiasi kikubwa kuongeza kipato na kupunguza umaskini.
Mhe Nasha Alisema kuwa uzalishaji wa
mazao, mifugo na uvuvi umeimarisha zaidi usalama wa chakula na lishe nchini, ambapo
katika mwaka 2015/2016 uzalishaji wa chakula ulikuwa ni tani milioni 16.2 ikiwa
ni ongezeko la tani milioni 0.7 (sawa na 4.5%)
ikilinganishwa na tani milioni 15.5 mwaka 2014/2015.
Uzalishaji wa mazao ya nafaka
umeongezeka kutoka tani milioni 8.9 mwaka 2014/ 2015 hadi tani milioni 9.5
mwaka 2015/ 2016 ikiwa ni ongezeko la tani milioni 0.6 (sawa na 6.7%). Uzalishaji wa mahindi umeongezeka kutoka tani
milioni 5.9 mwaka 2014/2015 hadi tani milioni 6.1 mwaka 2015/2016 sawa na
ongezeko la tani milioni 0.2 (sawa na 3.4%). Uzalishaji wa mchele uliongezeka
kutoka tani milioni 1.9 mwaka 2014/ 2015 hadi tani milioni 2.2 mwaka 2016 sawa
na ongezeko la tani milioni 0.3 (sawa na 15.8%).
Vilevile, uzalishaji wa mazao ya
chakula yasiyo nafaka umeongezeka hadi kufikia tani milioni 6.7 ikilinganishwa
na tani milioni 6.6 kwa mwaka 2014/ 2015 ikiwa ni sawa na ongezeko la tani
milioni 0.1 (sawa na 1.5%).
Kwa ujumla uzalishaji wa mazao ya
chakula ukilinganishwa na mahitaji ya tani milioni 13.2 ya chakula na matumizi
mengineyo katika mwaka 2016/2017 unaonesha kuwepo kwa ziada ya tani milioni 3.0
za chakula. Kutokana na hali hiyo Taifa limejitosheleza kwa chakula kwa
asilimia 123 ambayo ni ongezeko la asilimia 3 ikilinganishwa na asilimia 120 ya
mwaka 2015.
Katika mwaka 2016/2017 idadi ya mifugo
nchini imefikia ng’ombe milioni 28.44, mbuzi milioni 16.67 na kondoo milioni
5.01. Pia, wapo kuku wa asili milioni 37.43, kuku wa kisasa milioni 34.5,
nguruwe milioni 1.85 na punda wapatao
572,357. jumla ya mitamba 634 ilizalishwa kutoka mashamba ya Serikali na
Kampuni ya Ranchi za Taifa - NARCO ikilinganishwa na mitamba 646 iliyozalishwa
mwaka 2015/2016. Aidha, jumla ya mitamba 10,820 ilizalishwa na Sekta binafsi na
kusambazwa kwa wafugaji wadogo nchini ikilinganishwa na mitamba 10,803
iliyozalishwa mwaka 2015/2016.
Mhe Nasha alisema kuwa Vituo vya Kanda
vimeendelea kuimarishwa kwa kupatiwa vitendeakazi, ukarabati wa miundombinu na mitambo ili
kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya uhimilishaji wakati wote.
Jumla ya dozi 100,000 za mbegu bora za
mifugo zilizalishwa ikilinganishwa na dozi 80,000 mwaka 2015/2016. Pia, ng’ombe waliohimilishwa
wameongezeka kutoka 221,390 mwaka
2015/2016 hadi ng’ombe 457,557 mwaka 2016/2017.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia