Mkuu wa
Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, Crispin Meela (kulia) akipokea moja kati ya
msaada wa mashuka 100 yaliyotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa
ajili ya kutumiwa na wagonjwa wa hospitali ya mji wa Babati (Mrara)
anayemkabidhi ni meneja wa NHIF Mkoani humo, Isaya Shekifu.
Mkuu wa Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, Crispin Meela (kulia) akipokea msaada wa mashuka 100 yaliyotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa ajili ya kutumiwa na wagonjwa wa hospitali ya mji wa Babati (Mrara) anayemkabidhi ni meneja wa NHIF Mkoani Manyara, Isaya Shekifu.
Meneja wa Mfuko
wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Manyara, Isaya Shekifu akizungumza mara
baada ya kumkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Babati Crispin Meela mashuka 100
waliyotoa msaada kwenye hospitali ya mji wa Babati (Mrara), ambayo inakabiliwa
na upungufu wa mashuka kwa wagonjwa.
Mkuu wa
Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, Crispin Meela akizungumza mara baada ya
kupokea msaada wa mashuka 100 yaliyotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
(NHIF) kwa ajili ya kutumiwa na wagonjwa wa hospitali ya mji wa Babati (Mrara),
kushoto ni meneja wa NHIF mkoani humo, Isaya Shekifu na kulia ni Ofisa ushirika
wa halmashauri ya mji huo Keneth Shemdoe.
Habari picha na Woinde Shizza,Manyara
Hospitali ya
Mji wa Babati Mkoani Manyara, (Mrara) ambayo inakabiliwa na upungufu wa
mashuka, imekabidhiwa msaada wa mashuka 100 na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)
kwa ajili ya wagonjwa wanaolazwa hospitalini hapo.
Msaada huo wa
mashuka 100 ulikabidhiwa juzi kwa mkuu wa wilaya ya Babati Crispin Meela na Meneja
wa NHIF mkoani Manyara Isaya Shekifu, ambaye aliahidi kuongeza mashuka mengine
150 hivi karibuni kwenye hospitali hiyo.
Alisema wametoa
msaada huo mara baada ya kutembelea hospitali hiyo na kubaini upungufu mkubwa wa
mashuka yanayotumiwa na wagonjwa wanaolazwa kwenye wodi za hospitali hiyo ya
Mrara.
“Baada ya
kutoa mashuka haya 100, hivi karibuni tunatarajia kutoa mashuka mengine 150 ili
yawe 250 ambayo kwa kiasi kikubwa yatamaliza changamoto ya ukosefu wa mashuka kwa
wagonjwa wa hospitali hii,” alisema Shekifu.
Alisema wametoa
msaada huo mara baada ya kutembelea hospitali hiyo na kubaini upungufu mkubwa wa
mashuka yanayotumiwa na wagonjwa wanaolazwa kwenye wodi za hospitali hiyo ya
Mrara.
Naye, Meela
akizungumza mara baada ya kupokea mashuka hayo, aliushukuru uongozi wa NHIF
mkoani humo ambao walichukua muda mfupi wa kutoa msaada huo mara baada ya
kubaini kuwa kuna tatizo la upungufu wa mashuka.
"Hivi karibuni mimi na Shekifu tulitembelea hospitali ya Mrara na kubaini tatizo
kubwa la upungufu wa mashuka kwa wagonjwa na nilipotoa ombi hilo lilikubaliwa na
kutekelezwa kwa muda mfupi hivyo anawapongeza NHIF," alisema Meela.
Nao, baadhi
ya wakazi wa mji wa Babati walitoa ombi kwa asasi, taasisi, makampuni na mashirika
ya serikali na ya binafsi, kuiiga NHIF na kutoa mashuka mengine kwenye
hospitali hiyo ambayo ina uhaba wa mashuka kwa wagonjwa.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia