Ticker

6/recent/ticker-posts

KITAMBI NOMA YA TWAA UBIGWA WA SOKA KATIKA TAMASHA LA KWANZA LA AMANI NA UTALII JIJI ARUSHA

 Mwenyekiti wa kamati ya amani mkoa wa Arusha(APET) Petro Ahham
akimkabidhi kikombe cha ushindi  wa bonanza la amani na utalii mkoa wa
Arusha,nahodha wa timu ya Kitambi Noma, James Lugangira
 wanamichezo wa kitambinoma wakiwa wanashabikia ushindi mara baada ya kukabidhiwa kombe katika kiwanja cha General Tyre jijini Arusha




Na Woinde Shizza,Arusha

Klabu ya Kitambi noma ya jijini Arusha, juzi ilitwaa ubingwa wa soka
katika tamasha la kwanza la amani na utalii ambalo lilifanyika viwanja vya
General Tyre jijini Arusha.

Timu hiyo ilitwaa ubingwa baada ya kuzishinda timu za Wazee Klabu na chuo
cha Uandishi wa habari Arusha(AJTC) kwa kukusanya alama nyingi  kutokana na
mashindano yaliyoendeshwa kwa mfumo wa Ligi.

Katika tamasha hilo, liliandaliwa na taasisi ya Arusha media jumla ya timu
sita zilishiriki katika michezo mbali mbali na sambamba na kutolewa
burudani ya  ngoma za asili kutoka kikundi cha Cultural Arts Center cha
chuo kikuu cha Makumira

Hata hivyo kwa upande wa mpira wa pete, timu ya Wazee Qeen ilifanikiwa
kutwaa ubingwa baada ya kuichapa katika mchezo wa fainali timu ya AJTC Qeen
magoli 34-7.

Katika mchezo wa kukimbiza kuku, timu ya Kitambi noma ilishinda dhidi ya
Wazee Klabu na kwa upande wa wasichana AJTC ilishinda dhidi ya Wazee Qeen.

Akikabidhi zawadi za washindi , Mwenyekiti wa kamati ya amani mkoa wa
Arusha, Petro Ahham alipongeza timu zote zilizoshiriki kutokana kudumisha
amani kwa vitendo.

"tamasha hili limekuja wakati muafaka kwani Arusha ni jiji la kitalii
ambalo linahitaji amani wakati wote hivyo kufanya michezo kuhimiza amani na
utalii ni jambo jema sana"alisema

Awali Katibu wa chama cha soka wilaya ya Arusha,Zakhayo Mjema alipongeza
taasisi ya Arusha Media kwa kuandaa tamasha hilo la amani na utalii katika
jiji la Arusha.

"matamasha kama haya yalipaswa kufanywa na chama cha soka lakini tumekwama
hivyo, tunapongeza Arusha Media kwa kusaidia kuendeleza michezo katika jiji
la Arusha"alisema.

Tamasha hilo, lilidhaminiwa na Shirika la hifadhi za taifa(TANAPA),kampuni
ya vinywaji ya Cocacola, kampuni ya Sunny Safaris, kampuni ya Big
Expedition na kampuni ya Marera Lodge &tours.

Post a Comment

0 Comments